Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Quotations and Allusions: Matthew 12:18, »Behold my servant...«

9 mistari · 252 vipengele

Mistari kuhusu Matthew 12:18, »Behold my servant...«

  1. “Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye; nitaweka Roho yangu juu yake, naye ataleta haki kwa mataifa.

  2. Hatapaza sauti wala kupiga kelele, wala hataiinua sauti yake barabarani.

  3. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima. Kwa uaminifu ataleta haki,

  4. hatazimia roho wala kukata tamaa, mpaka atakaposimamisha haki juu ya dunia. Visiwa vitaweka tumaini lao katika sheria yake.”

  5. Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema:

  6. “Tazama mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Nitaweka Roho wangu juu yake, naye atatangaza haki kwa mataifa.

  7. Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani.

  8. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde.

  9. Katika Jina lake mataifa wataweka tumaini lao.”