Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Quotations and Allusions: Acts 2:17, »And it shall come to pass in the last days...«

11 mistari · 252 vipengele

Mistari kuhusu Acts 2:17, »And it shall come to pass in the last days...«

  1. “Hata itakuwa, baada ya hayo, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zenu watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.

  2. Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina Roho wangu.

  3. Nami nitaonyesha maajabu katika mbingu na duniani: damu, moto na mawimbi ya moshi.

  4. Jua litageuzwa kuwa giza na mwezi kuwa mwekundu kama damu, kabla ya kuja siku ya Bwana ile kuu na ya kutisha.

  5. Na kila mtu atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu kutakuwepo wokovu, kama Bwana alivyosema, miongoni mwa walionusurika ambao Bwana awaita.

  6. “ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.

  7. Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina Roho wangu, nao watatabiri.

  8. Nami nitaonyesha maajabu juu mbinguni, na ishara chini duniani: damu, moto, na mawimbi ya moshi.

  9. Jua litakuwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kuja siku ile kuu ya Bwana iliyo tukufu.

  10. Na kila mtu atakayeliitia jina la Bwana, ataokolewa.’

  11. Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa.”