Skip to content

circa 1446 BC

Moses & The Exodus

God raises up Moses to confront Pharaoh; the ten plagues culminate in Israel's dramatic deliverance from four centuries of bondage.

415 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli ambao walikwenda Misri na Yakobo, kila mmoja akiwa pamoja na jamaa yake:

  2. Reubeni, Simeoni, Lawi na Yuda;

  3. Isakari, Zabuloni na Benyamini;

  4. Dani na Naftali, Gadi na Asheri.

  5. Wazao wote wa Yakobo walikuwa watu sabini; Yosefu alikuwa tayari yuko Misri.

  6. Kutoka 1:6takriban 1635 KK

    Basi Yosefu na kaka zake wote na kizazi kile chote walikufa,

  7. Kutoka 1:7takriban 1635 KK

    lakini Waisraeli walikuwa wamezaana na kuongezeka sana, idadi yao ikawa kubwa mno, kwa hiyo wakaijaza nchi.

  8. Kutoka 1:8takriban 1635 KK

    Kisha mfalme mpya ambaye hakufahamu habari za Yosefu akatawala Misri.

  9. Kutoka 1:9takriban 1635 KK

    Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kutuliko sisi.

  10. Kutoka 1:10takriban 1635 KK

    Njooni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana dhidi yetu na kuondoka katika nchi hii.”

  11. Kutoka 1:11takriban 1635 KK

    Basi Wamisri wakaweka wasimamizi wa kuwasimamia na kuwatesa Waisraeli kwa kazi ngumu, nao wakajenga miji ya Pithomu na Ramesesi ya kuweka akiba ya Farao.

  12. Kutoka 1:12takriban 1635 KK

    Lakini walivyozidi kuteswa ndivyo walivyozidi kuongezeka na kuenea katika nchi; Wamisri wakawaogopa Waisraeli,

  13. Kutoka 1:13takriban 1635 KK

    kwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili.

  14. Kutoka 1:14takriban 1635 KK

    Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili.

  15. Kutoka 1:15takriban 1635 KK

    Mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kimisri waliowazalisha wanawake wa Kiebrania, ambao majina yao ni Shifra na Pua,

  16. Kutoka 1:16takriban 1635 KK

    “Mtakapowazalisha wanawake wa Kiebrania, chunguzeni wanapojifungua. Ikiwa ni mtoto wa kiume, muueni, lakini ikiwa ni msichana, mwacheni aishi.”

  17. Kutoka 1:17takriban 1635 KK

    Lakini hao wakunga walimcha Mungu na hawakufanya kile mfalme wa Misri alichowaambia kufanya, bali wakawaacha watoto wa kiume waishi.

  18. Kutoka 1:18takriban 1635 KK

    Ndipo mfalme wa Misri akawaita hao wakunga, akawauliza, “Kwa nini mmefanya hivi? Mbona mmeacha watoto wa kiume waishi?”

  19. Kutoka 1:19takriban 1635 KK

    Wakunga wakamjibu Farao, “Wanawake wa Kiebrania ni tofauti na wanawake wa Kimisri; wao wana nguvu, nao hujifungua watoto kabla wakunga hawajafika.”

  20. Kutoka 1:20takriban 1635 KK

    Kwa hiyo Mungu akawatendea mema wakunga hao. Waisraeli wakaongezeka na kuendelea kuwa wengi zaidi.

  21. Kutoka 1:21takriban 1635 KK

    Kwa vile hao wakunga walimcha Mungu, Mungu akawajalia kuwa na jamaa zao wenyewe.

  22. Kutoka 1:22takriban 1573 KK

    Kisha Farao akatoa agizo hili kwa watu wake wote: “Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa kwa Waebrania lazima atupwe katika Mto Naili, bali kila mtoto wa kike aachwe aishi.”

  23. Kutoka 2:1takriban 1572 KK

    Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi,

  24. Kutoka 2:2takriban 1571 KK

    naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu.

  25. Kutoka 2:3takriban 1571 KK

    Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili.