Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Quotations and Allusions: 1 Peter 3:10, »For he that will love life...«

8 mistari · 252 vipengele

Mistari kuhusu 1 Peter 3:10, »For he that will love life...«

  1. Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema,

  2. basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo.

  3. Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.

  4. Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.

  5. Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu, ili kufuta kumbukumbu lao duniani.

  6. Kwa maana, “Yeyote apendaye uzima na kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila.

  7. Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.

  8. Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza maombi yao. Bali uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu.”