- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1446–1406 BC
The Wilderness Years
Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.
Mistari ya kipindi hiki
- Hesabu 1:1takriban 1490 KK
Bwana alisema na Mose katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia,
- Hesabu 1:2takriban 1490 KK
“Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja.
- Hesabu 1:3takriban 1490 KK
Wewe na Aroni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea ambao wanaweza kutumika katika jeshi.
- Hesabu 1:4takriban 1490 KK
Mwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia.
- Hesabu 1:5takriban 1490 KK
Haya ndiyo majina ya wanaume watakaowasaidia: “kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;
- Hesabu 1:6takriban 1490 KK
kutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;
- Hesabu 1:7takriban 1490 KK
kutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;
- Hesabu 1:8takriban 1490 KK
kutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;
- Hesabu 1:9takriban 1490 KK
kutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;
- Hesabu 1:10takriban 1490 KK
kutoka wana wa Yosefu: kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi; kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri;
- Hesabu 1:11takriban 1490 KK
kutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;
- Hesabu 1:12takriban 1490 KK
kutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;
- Hesabu 1:13takriban 1490 KK
kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;
- Hesabu 1:14takriban 1490 KK
kutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;
- Hesabu 1:15takriban 1490 KK
kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”
- Hesabu 1:16takriban 1490 KK
Hawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli.
- Hesabu 1:17takriban 1490 KK
Mose na Aroni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao,
- Hesabu 1:18takriban 1490 KK
wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonyesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja,
- Hesabu 1:19takriban 1490 KK
kama Bwana alivyomwagiza Mose. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:
- Hesabu 1:20takriban 1490 KK
Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
- Hesabu 1:21takriban 1490 KK
Idadi kutoka kabila la Reubeni ilikuwa watu 46,500.
- Hesabu 1:22takriban 1490 KK
Kutoka wazao wa Simeoni: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
- Hesabu 1:23takriban 1490 KK
Idadi kutoka kabila la Simeoni walikuwa watu 59,300.
- Hesabu 1:24takriban 1490 KK
Kutoka wazao wa Gadi: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
- Hesabu 1:25takriban 1490 KK
Idadi kutoka kabila la Gadi walikuwa watu 45,650.