Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kumbukumbu 33:20takriban 1451 KK

    Kuhusu Gadi akasema: “Atabarikiwa yeye aongezaye milki ya Gadi! Gadi huishi huko kama simba, akirarua kwenye mkono au kichwa.

  2. Kumbukumbu 33:21takriban 1451 KK

    Alijichagulia nchi nzuri kuliko zote kwa ajili yake mwenyewe; fungu la kiongozi lilikuwa limehifadhiwa kwa ajili yake. Viongozi wa watu walipokusanyika, alitimiza haki ya mapenzi ya Bwana, na hukumu zake kuhusu Israeli.”

  3. Kumbukumbu 33:22takriban 1451 KK

    Kuhusu Dani akasema: “Dani ni mwana simba, akiruka kutoka Bashani.”

  4. Kumbukumbu 33:23takriban 1451 KK

    Kuhusu Naftali akasema: “Naftali amejaa tele upendeleo wa Bwana, naye amejaa baraka yake; atarithi magharibi na kusini.”

  5. Kumbukumbu 33:24takriban 1451 KK

    Kuhusu Asheri akasema: “Aliyebarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri; yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake, yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta.

  6. Kumbukumbu 33:25takriban 1451 KK

    Makomeo ya malango yako yawe chuma na shaba, nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako.

  7. Kumbukumbu 33:26takriban 1451 KK

    “Hakuna mwingine kama Mungu wa Yeshuruni, ambaye hupanda juu ya mbingu ili akusaidie, na juu ya mawingu katika utukufu wake.

  8. Kumbukumbu 33:27takriban 1451 KK

    Mungu wa milele ni kimbilio lako, na chini kuna mikono ya milele. Atamfukuza adui yako mbele yako, akisema, ‘Mwangamize yeye!’

  9. Kumbukumbu 33:28takriban 1451 KK

    Hivyo Israeli ataishi salama peke yake. Mzao wa Yakobo ni salama katika nchi ya nafaka na divai mpya, mahali ambapo mbingu hudondosha umande.

  10. Kumbukumbu 33:29takriban 1451 KK

    Ee Israeli, wewe umebarikiwa! Ni nani kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana? Yeye ni ngao yako na msaada wako, na upanga wako uliotukuka. Adui zako watatetemeka mbele yako, nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.”

  11. Kumbukumbu 34:1takriban 1451 KK

    Kisha Mose akaupanda mlima Nebo kutoka tambarare za Moabu mpaka kilele cha Pisga, ngʼambo ya Yeriko. Huko Bwana akamwonyesha nchi yote: kutoka Gileadi mpaka Dani,

  12. Kumbukumbu 34:2takriban 1451 KK

    Naftali yote, nchi ya Efraimu na Manase, nchi yote ya Yuda mpaka bahari ya magharibi,

  13. Kumbukumbu 34:3takriban 1451 KK

    Negebu na nchi yote kuanzia Bonde la Yeriko, Mji wa Mitende, hadi Soari.

  14. Kumbukumbu 34:4takriban 1451 KK

    Kisha Bwana akamwambia, “Hii ndiyo nchi niliyomwahidi Abrahamu na Isaki na Yakobo kwa kiapo niliposema, ‘Nitawapa wazao wako.’ Nimekuruhusu uione kwa macho yako, lakini hutavuka kuingia.”

  15. Kumbukumbu 34:5takriban 1451 KK

    Naye Mose mtumishi wa Bwana akafa huko Moabu, kama Bwana alivyokuwa amesema.

  16. Kumbukumbu 34:6takriban 1451 KK

    Mungu akamzika huko Moabu, katika bonde mkabala na Beth-Peori, lakini hakuna ajuaye kaburi lake lilipo mpaka leo.

  17. Kumbukumbu 34:7takriban 1451 KK

    Mose alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; hata hivyo nguvu ya macho yake haikufifia wala mwili wake haukudhoofika.

  18. Kumbukumbu 34:8takriban 1451 KK

    Waisraeli wakaomboleza kwa ajili ya Mose kwenye tambarare za Moabu kwa siku thelathini, mpaka wakati wa kulia na kuomboleza ulipopita.

  19. Kumbukumbu 34:9takriban 1451 KK

    Basi Yoshua mwana wa Nuni alijazwa roho ya hekima kwa sababu Mose alikuwa ameweka mikono yake juu yake. Kwa hiyo Waisraeli wakamsikiliza na wakafanya yale ambayo Bwana alikuwa amemwagiza Mose.

  20. Kumbukumbu 34:10takriban 1451 KK

    Tangu wakati huo, katika Israeli hajainuka nabii mwingine kama Mose, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso,

  21. Kumbukumbu 34:11takriban 1451 KK

    aliyetenda ishara zote zile za miujiza na maajabu ambayo Bwana alimtuma kuyatenda huko Misri, yaani kwa Farao na maafisa wake wote na nchi yake yote.

  22. Kumbukumbu 34:12takriban 1451 KK

    Kwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyewahi kuonyesha nguvu nyingi ama kutenda matendo ya kutisha ambayo Mose aliwahi kuyafanya mbele ya Israeli yote.