Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Siyo maneno matupu tu kwenu, bali ni uzima wenu. Kwa hayo mtaishi maisha marefu katika nchi mnayovuka Yordani kuimiliki.”

  2. Kumbukumbu 32:48takriban 1451 KK

    Siku hiyo hiyo Bwana akamwambia Mose,

  3. Kumbukumbu 32:49takriban 1451 KK

    “Kwea katika mapangano ya Mlima Abarimu hadi kilima cha Nebo kilichoko Moabu, ngʼambo ya Yeriko, na uitazame Kanaani, nchi ninayowapa Waisraeli kama milki yao wenyewe.

  4. Kumbukumbu 32:50takriban 1451 KK

    Utafia kwenye mlima huo unaokwea na kukusanyika pamoja na watu wako, kama ndugu yako Aroni alivyofia juu ya Mlima Hori naye akakusanyika kwa watu wake.

  5. Kumbukumbu 32:51takriban 1451 KK

    Hii ni kwa sababu ninyi wawili mlivunja uaminifu nami mbele ya Waisraeli kwenye maji ya Meriba-Kadeshi katika Jangwa la Sini, na kwa sababu hamkuuinua utakatifu wangu miongoni mwa Waisraeli.

  6. Kumbukumbu 32:52takriban 1451 KK

    Kwa hiyo, utaiona tu nchi kwa mbali; wewe hutaingia nchi ninayowapa watu wa Israeli.”

  7. Kumbukumbu 33:1takriban 1451 KK

    Hii ndiyo baraka Mose mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake.

  8. Kumbukumbu 33:2takriban 1451 KK

    Alisema: “Bwana alikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka materemko ya mlima wake.

  9. Kumbukumbu 33:3takriban 1451 KK

    Hakika ni wewe ambaye huwapenda watu, watakatifu wako wote wamo mkononi mwako. Miguuni pako wote wanasujudu na kutoka kwako wanapokea mafundisho,

  10. Kumbukumbu 33:4takriban 1451 KK

    sheria ile Mose aliyotupa sisi, tulio milki ya kusanyiko la Yakobo.

  11. Kumbukumbu 33:5takriban 1451 KK

    Alikuwa mfalme juu ya Yeshuruni wakati viongozi wa watu walipokusanyika, pamoja na makabila ya Israeli.

  12. Kumbukumbu 33:6takriban 1451 KK

    “Reubeni na aishi, asife, wala watu wake wasiwe wachache.”

  13. Kumbukumbu 33:7takriban 1451 KK

    Akasema hili kuhusu Yuda: “Ee Bwana, sikia kilio cha Yuda, mlete kwa watu wake. Kwa mikono yake mwenyewe hujitetea. Naam, uwe msaada wake dhidi ya adui zake!”

  14. Kumbukumbu 33:8takriban 1451 KK

    Kuhusu Lawi alisema: “Thumimu yako na Urimu yako ulimpa, mtu yule uliyemfadhili. Ulimjaribu huko Masa na kushindana naye kwenye maji ya Meriba.

  15. Kumbukumbu 33:9takriban 1451 KK

    Alinena hivi kuhusu baba yake na mama yake, ‘Mimi siwahitaji kamwe.’ Akawasahau jamaa zake, asiwatambue hata watoto wake, lakini akaliangalia neno lako na kulilinda Agano lako.

  16. Kumbukumbu 33:10takriban 1451 KK

    Humfundisha Yakobo mausia yako na Israeli sheria yako. Hufukiza uvumba mbele zako na sadaka nzima za kuteketezwa juu ya madhabahu yako.

  17. Kumbukumbu 33:11takriban 1451 KK

    Ee Bwana, bariki ustadi wake wote, nawe upendezwe na kazi ya mikono yake. Vipige viuno vya wale wainukao dhidi yake; wapige adui zake hata wasiinuke tena.”

  18. Kumbukumbu 33:12takriban 1451 KK

    Kuhusu Benyamini akasema: “Mwache mpenzi wa Bwana apumzike salama kwake, kwa maana humkinga mchana kutwa, na yule Bwana ampendaye hupumzika kati ya mabega yake.”

  19. Kumbukumbu 33:13takriban 1451 KK

    Kuhusu Yosefu akasema: “Bwana na aibariki nchi yake kwa umande wa thamani kutoka mbinguni juu, na vilindi vya maji vilivyotulia chini;

  20. Kumbukumbu 33:14takriban 1451 KK

    pamoja na vitu vilivyo bora sana viletwavyo na jua, na vitu vizuri sana vinavyoweza kutolewa na mwezi;

  21. Kumbukumbu 33:15takriban 1451 KK

    pamoja na zawadi bora sana za milima ya zamani na kwa wingi wa baraka za vilima vya milele;

  22. Kumbukumbu 33:16takriban 1451 KK

    pamoja na baraka nzuri mno za ardhi na ukamilifu wake, na upendeleo wake yeye aliyeishi kwenye kichaka kilichokuwa kinawaka moto. Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji la uso la aliye mkuu miongoni mwa ndugu zake.

  23. Kumbukumbu 33:17takriban 1451 KK

    Katika fahari yeye ni kama fahali mzaliwa wa kwanza; pembe zake ni pembe za nyati, na kwa pembe hizo atapiga mataifa, hata yaliyo miisho ya dunia. Hivyo ndivyo yalivyo makumi elfu ya Efraimu; hivyo ndivyo yalivyo maelfu ya Manase.”

  24. Kumbukumbu 33:18takriban 1451 KK

    Kuhusu Zabuloni akasema: “Shangilia, Zabuloni, wakati wa kutoka nje, nawe Isakari, katika mahema yako.

  25. Kumbukumbu 33:19takriban 1451 KK

    Watawaita mataifa kwenye mlima, na huko mtatoa dhabihu za haki; watajifurahisha kwa wingi uliojaza bahari, kwa hazina zilizofichwa mchangani.”