Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 1:51takriban 1490 KK

    Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.

  2. Hesabu 1:52takriban 1490 KK

    Waisraeli watapiga mahema yao kwa makundi makundi, kila mwanaume katika kambi yake mwenyewe chini ya bendera yake.

  3. Hesabu 1:53takriban 1490 KK

    Hata hivyo, Walawi watapiga mahema yao kuzunguka Maskani ya Ushuhuda ili ghadhabu isiipate jumuiya ya Waisraeli. Walawi watawajibika kwa utunzaji wa Maskani ya Ushuhuda.”

  4. Hesabu 1:54takriban 1490 KK

    Waisraeli walifanya yote haya sawasawa kama Bwana alivyomwamuru Mose.

  5. Hesabu 2:1takriban 1490 KK

    Bwana aliwaambia Mose na Aroni:

  6. Hesabu 2:2takriban 1490 KK

    “Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali fulani kutoka kwenye hema, kila mwanaume chini ya alama yake pamoja na bendera ya jamaa yake.”

  7. Hesabu 2:3takriban 1490 KK

    Kwa upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu.

  8. Hesabu 2:4takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 74,600.

  9. Hesabu 2:5takriban 1490 KK

    Kabila la Isakari watapiga kambi karibu na Yuda. Kiongozi wa watu wa Isakari ni Nethaneli mwana wa Suari.

  10. Hesabu 2:6takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 54,400.

  11. Hesabu 2:7takriban 1490 KK

    Kabila la Zabuloni litafuata. Kiongozi wa watu wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni.

  12. Hesabu 2:8takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 57,400.

  13. Hesabu 2:9takriban 1490 KK

    Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kuondoka.

  14. Hesabu 2:10takriban 1490 KK

    Kwa upande wa kusini kutakuwa kambi ya makundi ya Reubeni chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Reubeni ni Elisuri mwana wa Shedeuri.

  15. Hesabu 2:11takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 46,500.

  16. Hesabu 2:12takriban 1490 KK

    Kabila la Simeoni watapiga kambi karibu na Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Surishadai.

  17. Hesabu 2:13takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 59,300.

  18. Hesabu 2:14takriban 1490 KK

    Kabila la Gadi litafuata. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli.

  19. Hesabu 2:15takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 45,650.

  20. Hesabu 2:16takriban 1490 KK

    Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni 151,450. Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka.

  21. Hesabu 2:17takriban 1490 KK

    Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.

  22. Hesabu 2:18takriban 1490 KK

    Upande wa magharibi kutakuwepo na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.

  23. Hesabu 2:19takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 40,500.

  24. Hesabu 2:20takriban 1490 KK

    Kabila la Manase litafuata baada ya Efraimu. Kiongozi wa watu wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri.

  25. Hesabu 2:21takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 32,200.