Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 2:22takriban 1490 KK

    Kabila la Benyamini litafuata baada ya Manase. Kiongozi wa watu wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni.

  2. Hesabu 2:23takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 35,400.

  3. Hesabu 2:24takriban 1490 KK

    Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.

  4. Hesabu 2:25takriban 1490 KK

    Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.

  5. Hesabu 2:26takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 62,700.

  6. Hesabu 2:27takriban 1490 KK

    Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani.

  7. Hesabu 2:28takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 41,500.

  8. Hesabu 2:29takriban 1490 KK

    Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.

  9. Hesabu 2:30takriban 1490 KK

    Kundi lake lina watu 53,400.

  10. Hesabu 2:31takriban 1490 KK

    Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni 157,600. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya alama yao.

  11. Hesabu 2:32takriban 1490 KK

    Hawa ndio Waisraeli, wakiwa wamehesabiwa kufuatana na jamaa zao. Wote walio kambini kwa makundi yao ni watu 603,550.

  12. Hesabu 2:33takriban 1490 KK

    Hata hivyo, Walawi hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

  13. Hesabu 2:34takriban 1490 KK

    Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu Bwana alichomwamuru Mose. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.

  14. Hesabu 3:1takriban 1490 KK

    Hii ni hesabu ya jamaa ya Aroni na Mose kwa wakati ambao Bwana alizungumza na Mose katika Mlima Sinai.

  15. Hesabu 3:2takriban 1490 KK

    Majina ya wana wa Aroni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari.

  16. Hesabu 3:3takriban 1490 KK

    Hayo yalikuwa majina ya wana wa Aroni, makuhani wapakwa mafuta, waliokuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani.

  17. Hesabu 3:4takriban 1490 KK

    Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Aroni baba yao.

  18. Hesabu 3:5takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  19. Hesabu 3:6takriban 1490 KK

    “Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie.

  20. Hesabu 3:7takriban 1490 KK

    Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani.

  21. Hesabu 3:8takriban 1490 KK

    Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.

  22. Hesabu 3:9takriban 1490 KK

    Wakabidhi Walawi kwa Aroni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kwake kabisa.

  23. Hesabu 3:10takriban 1490 KK

    Waweke Aroni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine yeyote atakayesogea mahali patakatifu ni lazima auawe.”

  24. Hesabu 3:11takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  25. Hesabu 3:12takriban 1490 KK

    “Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu,