Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 3:13takriban 1490 KK

    kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana.”

  2. Hesabu 3:14takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose katika Jangwa la Sinai,

  3. Hesabu 3:15takriban 1490 KK

    “Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”

  4. Hesabu 3:16takriban 1490 KK

    Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Bwana.

  5. Hesabu 3:17takriban 1490 KK

    Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

  6. Hesabu 3:18takriban 1490 KK

    Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni: Libni na Shimei.

  7. Hesabu 3:19takriban 1490 KK

    Koo za Wakohathi zilikuwa ni: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

  8. Hesabu 3:20takriban 1490 KK

    Koo za Wamerari zilikuwa ni: Mahli na Mushi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.

  9. Hesabu 3:21takriban 1490 KK

    Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagershoni.

  10. Hesabu 3:22takriban 1490 KK

    Idadi ya waume wote waliokuwa na mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 7,500.

  11. Hesabu 3:23takriban 1490 KK

    Ukoo wa Wagershoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani.

  12. Hesabu 3:24takriban 1490 KK

    Kiongozi wa jamaa za Wagershoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli.

  13. Hesabu 3:25takriban 1490 KK

    Katika Hema la Kukutania, Wagershoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania,

  14. Hesabu 3:26takriban 1490 KK

    mapazia ya ua, pazia katika ingilio la ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.

  15. Hesabu 3:27takriban 1490 KK

    Kwa Kohathi kulikuwepo koo za Waamramu, Waishari, Wahebroni na Wauzieli; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wakohathi.

  16. Hesabu 3:28takriban 1490 KK

    Hesabu ya waume wote wenye mwezi mmoja au zaidi ilikuwa watu 8,600. Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu.

  17. Hesabu 3:29takriban 1490 KK

    Koo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani.

  18. Hesabu 3:30takriban 1490 KK

    Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli.

  19. Hesabu 3:31takriban 1490 KK

    Waliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake.

  20. Hesabu 3:32takriban 1490 KK

    Kiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Aroni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.

  21. Hesabu 3:33takriban 1490 KK

    Kwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari.

  22. Hesabu 3:34takriban 1490 KK

    Hesabu ya waume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 6,200.

  23. Hesabu 3:35takriban 1490 KK

    Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.

  24. Hesabu 3:36takriban 1490 KK

    Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake,

  25. Hesabu 3:37takriban 1490 KK

    na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.