Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 4:12takriban 1490 KK

    “Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika kuhudumia mahali patakatifu, watavisokotea kwenye kitambaa cha buluu na kufunika kwa ngozi za pomboo, na kuviweka juu ya miti ya kuchukulia.

  2. Hesabu 4:13takriban 1490 KK

    “Wataondoa majivu kutoka madhabahu ya shaba na kutandaza kitambaa cha zambarau juu yake.

  3. Hesabu 4:14takriban 1490 KK

    Kisha wataweka vyombo vyote juu yake vinavyotumika kwa kuhudumia madhabahuni pamoja na vyombo vya kutolea moto, nyuma, miiko na mabakuli ya kunyunyizia. Juu yake watatandaza ngozi za pomboo ya kufunika, na kuweka mipiko mahali pake.

  4. Hesabu 4:15takriban 1490 KK

    “Baada ya Aroni na wanawe kumaliza kazi ya kufunika samani takatifu na vyombo vyake vyote, watu watakapokuwa tayari kungʼoa kambi, Wakohathi watakuja kufanya kazi ya kubeba. Lakini wasije wakagusa vitu vitakatifu la sivyo watakufa. Wakohathi ndio watakaobeba vile vitu vilivyomo katika Hema la Kukutania.

  5. Hesabu 4:16takriban 1490 KK

    “Eleazari mwana wa Aroni, kuhani, ndiye atakayesimamia mafuta kwa ajili ya taa, uvumba wenye harufu nzuri, sadaka za kila siku za nafaka na mafuta ya upako. Ndiye atakayekuwa msimamizi wa maskani yote ya Bwana na kila kitu kilichomo ndani mwake pamoja na samani takatifu na vyombo vyake.”

  6. Hesabu 4:17takriban 1490 KK

    Bwana akawaambia Mose na Aroni,

  7. Hesabu 4:18takriban 1490 KK

    “Hakikisheni kwamba koo za kabila la Wakohathi hawatengwi kutoka Walawi.

  8. Hesabu 4:19takriban 1490 KK

    Ili wapate kuishi wala wasife wanapokaribia vitu vitakatifu sana, uwafanyie hivi: Aroni na wanawe watakwenda mahali patakatifu na kumgawia kila mtu kazi yake, na kwamba ni nini atakachochukua.

  9. Hesabu 4:20takriban 1490 KK

    Lakini Wakohathi hawaruhusiwi kuingia ndani ili kuangalia vitu vitakatifu, hata kwa kitambo kidogo, la sivyo watakufa.”

  10. Hesabu 4:21takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  11. Hesabu 4:22takriban 1490 KK

    “Wahesabu pia Wagershoni kwa jamaa zao na koo zao.

  12. Hesabu 4:23takriban 1490 KK

    Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao huja kutumika katika Hema la Kukutania.

  13. Hesabu 4:24takriban 1490 KK

    “Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni wakati wanapofanya kazi na kubeba mizigo.

  14. Hesabu 4:25takriban 1490 KK

    Watabeba mapazia ya maskani. Hema la Kukutania, kifuniko chake na kifuniko cha nje cha ngozi za pomboo, mapazia ya maingilio ya Hema la Kukutania,

  15. Hesabu 4:26takriban 1490 KK

    mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagershoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi.

  16. Hesabu 4:27takriban 1490 KK

    Utumishi wao wote ukiwa ni kuchukua au wa kufanya kazi nyingine, utafanyika chini ya maelekezo ya Aroni na wanawe. Mtawapangia kama wajibu wao yote watakayoyafanya.

  17. Hesabu 4:28takriban 1490 KK

    Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni katika Hema la Kukutania. Wajibu wao utakuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani Aroni.

  18. Hesabu 4:29takriban 1490 KK

    “Wahesabu Wamerari kwa koo zao na jamaa zao.

  19. Hesabu 4:30takriban 1490 KK

    Wahesabu wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao watakuja kutumika katika Hema la Kukutania.

  20. Hesabu 4:31takriban 1490 KK

    Huu ndio wajibu wao wanapofanya huduma katika Hema la Kukutania: kubeba miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo na vitako,

  21. Hesabu 4:32takriban 1490 KK

    nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema, kamba, vifaa vyake vyote na kila kitu kinachohusiana na matumizi yake. Kila mtu mpangie vitu maalum vya kubeba.

  22. Hesabu 4:33takriban 1490 KK

    Huu ndio utumishi wa koo za Merari kama watakavyofanya kazi katika Hema la Kukutania, chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni.”

  23. Hesabu 4:34takriban 1490 KK

    Mose, Aroni na viongozi wa jumuiya wakawahesabu Wakohathi kwa koo zao na jamaa zao.

  24. Hesabu 4:35takriban 1490 KK

    Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

  25. Hesabu 4:36takriban 1490 KK

    waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 2,750.