Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 4:37takriban 1490 KK

    Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wote wale wa koo za Wakohathi ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri ya Bwana kupitia kwa Mose.

  2. Hesabu 4:38takriban 1490 KK

    Wagershoni walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao.

  3. Hesabu 4:39takriban 1490 KK

    Watu wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

  4. Hesabu 4:40takriban 1490 KK

    waliohesabiwa kwa koo zao na jamaa zao, walikuwa 2,630.

  5. Hesabu 4:41takriban 1490 KK

    Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wale wa koo za Gershoni ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri ya Bwana.

  6. Hesabu 4:42takriban 1490 KK

    Wamerari walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao.

  7. Hesabu 4:43takriban 1490 KK

    Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

  8. Hesabu 4:44takriban 1490 KK

    waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 3,200.

  9. Hesabu 4:45takriban 1490 KK

    Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wale wa koo za Wamerari. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatia amri ya Bwana kupitia kwa Mose.

  10. Hesabu 4:46takriban 1490 KK

    Hivyo Mose, Aroni na viongozi wa Israeli waliwahesabu Walawi wote kwa koo zao na jamaa zao.

  11. Hesabu 4:47takriban 1490 KK

    Wanaume wote wenye umri kuanzia miaka thelathini hadi hamsini waliokuja kufanya kazi ya kuhudumu na kubeba Hema la Kukutania

  12. Hesabu 4:48takriban 1490 KK

    walikuwa watu 8,580.

  13. Hesabu 4:49takriban 1490 KK

    Kwa amri ya Bwana kupitia Mose, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba. Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kama Bwana alivyomwamuru Mose.

  14. Hesabu 5:1takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  15. Hesabu 5:2takriban 1490 KK

    “Waamuru Waisraeli kumtoa nje ya kambi mtu yeyote ambaye ana ugonjwa wa ngozi uambukizao, au anayetokwa na majimaji ya aina yoyote, au ambaye ni najisi kwa utaratibu wa ibada kwa sababu ya maiti.

  16. Hesabu 5:3takriban 1490 KK

    Hii itakuwa ni kwa wote, yaani, wanaume na wanawake; watoeni nje ya kambi ili wasije wakanajisi kambi yao, ambamo ninaishi miongoni mwao.”

  17. Hesabu 5:4takriban 1490 KK

    Waisraeli wakafanya hivyo; wakawatoa nje ya kambi. Wakafanya kama vile Bwana alivyokuwa amemwelekeza Mose.

  18. Hesabu 5:5takriban 1490 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  19. Hesabu 5:6takriban 1490 KK

    “Waambie Waisraeli, ‘Wakati mwanaume au mwanamke akimkosea mwenzake kwa njia yoyote, na kwa hivyo akawa si mwaminifu kwa Bwana, mtu huyo ana hatia,

  20. Hesabu 5:7takriban 1490 KK

    na ni lazima atubu dhambi aliyoifanya. Ni lazima atoe malipo kamili kwa ajili ya kosa lake, aongeze sehemu ya tano juu ya malipo hayo na kutoa yote kwa mtu aliyemkosea.

  21. Hesabu 5:8takriban 1490 KK

    Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye malipo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kosa, malipo yatakuwa mali ya Bwana, nayo ni lazima apewe kuhani, pamoja na kondoo dume ambaye anatumika kufanyia upatanisho kwa ajili yake.

  22. Hesabu 5:9takriban 1490 KK

    Matoleo yote matakatifu ya Waisraeli wanayoleta kwa kuhani yatakuwa yake.

  23. Hesabu 5:10takriban 1490 KK

    Kila kitu cha mtu kilichowekwa wakfu ni chake mwenyewe, lakini kile atoacho kwa kuhani kitakuwa cha kuhani.’ ”

  24. Hesabu 5:11takriban 1490 KK

    Kisha Bwana akamwambia Mose,

  25. Hesabu 5:12takriban 1490 KK

    “Nena na Waisraeli uwaambie: ‘Ikiwa mke wa mtu amepotoka na si mwaminifu kwa mumewe,