- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa AD 48–96
Letters to the Churches
Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.
Mistari ya kipindi hiki
- 1 Wakorintho 11:31takriban 59 BK
Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingehukumiwa.
- 1 Wakorintho 11:32takriban 59 BK
Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadibishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.
- 1 Wakorintho 11:33takriban 59 BK
Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo pamoja ili kula, mngojane.
- 1 Wakorintho 11:34takriban 59 BK
Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani kwake ili mkutanapo pamoja msije mkahukumiwa. Nami nitakapokuja nitawapa maelekezo zaidi.
- 1 Wakorintho 12:1takriban 59 BK
Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu.
- 1 Wakorintho 12:2takriban 59 BK
Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au ingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena.
- 1 Wakorintho 12:3takriban 59 BK
Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu.
- 1 Wakorintho 12:4takriban 59 BK
Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule.
- 1 Wakorintho 12:5takriban 59 BK
Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule.
- 1 Wakorintho 12:6takriban 59 BK
Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.
- 1 Wakorintho 12:7takriban 59 BK
Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.
- 1 Wakorintho 12:8takriban 59 BK
Maana mtu mmoja kwa Roho hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kwa Roho huyo huyo.
- 1 Wakorintho 12:9takriban 59 BK
Mtu mwingine imani kwa huyo Roho na mwingine karama za kuponya kwa huyo Roho mmoja.
- 1 Wakorintho 12:10takriban 59 BK
Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua roho, kwa mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingine bado, tafsiri za lugha.
- 1 Wakorintho 12:11takriban 59 BK
Haya yote hufanywa na huyo huyo Roho mmoja, Roho naye humgawia kila mtu, kama apendavyo.
- 1 Wakorintho 12:12takriban 59 BK
Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo.
- 1 Wakorintho 12:13takriban 59 BK
Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
- 1 Wakorintho 12:14takriban 59 BK
Basi mwili si kiungo kimoja, bali ni viungo vingi.
- 1 Wakorintho 12:15takriban 59 BK
Kama mguu ungesema, “Kwa kuwa mimi si mkono basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya huo mguu usiwe sehemu ya mwili.
- 1 Wakorintho 12:16takriban 59 BK
Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili.
- 1 Wakorintho 12:17takriban 59 BK
Kama mwili wote ungelikuwa jicho, kusikia kungekuwa wapi? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, kunusa kungekuwa wapi?
- 1 Wakorintho 12:18takriban 59 BK
Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda.
- 1 Wakorintho 12:19takriban 59 BK
Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
- 1 Wakorintho 12:20takriban 59 BK
Kama ulivyo, una viungo vingi, lakini mwili ni mmoja.
- 1 Wakorintho 12:21takriban 59 BK
Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sina haja nawe!” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sina haja na ninyi!”