Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Timotheo 1:1takriban 65 BK

    Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Kristo Yesu tumaini letu.

  2. 1 Timotheo 1:2takriban 65 BK

    Kwa Timotheo, mwanangu halisi katika imani: Neema, rehema na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

  3. 1 Timotheo 1:3takriban 65 BK

    Kama nilivyokusihi wakati nilipokwenda Makedonia, endelea kubaki Efeso, ili kwamba upate kuwaagiza watu wasiendelee kufundisha mafundisho ya uongo

  4. 1 Timotheo 1:4takriban 65 BK

    wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani.

  5. 1 Timotheo 1:5takriban 65 BK

    Kusudi la maagizo haya ni upendo utokao katika moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli.

  6. 1 Timotheo 1:6takriban 65 BK

    Watu wengine wamepotoka kutoka haya na kugeukia majadiliano yasiyo na maana kwa kuwa,

  7. 1 Timotheo 1:7takriban 65 BK

    wanataka kuwa walimu wa sheria, lakini hawajui mambo yale wanayosema wala hayo wanayoyatumainia kwa uthabiti.

  8. 1 Timotheo 1:8takriban 65 BK

    Tunajua kwamba sheria ni njema ikiwa inatumika kwa halali kama ilivyokusudiwa.

  9. 1 Timotheo 1:9takriban 65 BK

    Lakini tunajua ya kuwa sheria si kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, kwa ajili ya wasiomcha Mungu na wenye dhambi, wasio watakatifu na wanaokufuru; kwa wale wawauao baba zao au mama zao, kwa wauaji,

  10. 1 Timotheo 1:10takriban 65 BK

    kwa wazinzi na wahanithi, kwa wale wauzao watu, na kwa waongo na waapao kwa uongo, na kwa chochote kingine kilicho kinyume na mafundisho ya kweli,

  11. 1 Timotheo 1:11takriban 65 BK

    ambayo yanakubaliana na Injili ya utukufu wa Mungu anayehimidiwa, ambayo mimi nimewekewa amana.

  12. 1 Timotheo 1:12takriban 65 BK

    Namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona mwaminifu, akaniteua kwa kazi yake.

  13. 1 Timotheo 1:13takriban 65 BK

    Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri, lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutojua na kutoamini kwangu.

  14. 1 Timotheo 1:14takriban 65 BK

    Neema ya Bwana wetu ilimiminwa juu yangu kwa wingi, ikiambatana na imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.

  15. 1 Timotheo 1:15takriban 65 BK

    Msemo huu ni wa kweli na unaostahili kukubalika, usemao kwamba: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi, ambao mimi ndiye niliye mbaya kuliko wote.

  16. 1 Timotheo 1:16takriban 65 BK

    Lakini kwa sababu hiyo nilipata rehema, ili katika mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo Yesu apate kuonyesha uvumilivu wake usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini na wapate uzima wa milele.

  17. 1 Timotheo 1:17takriban 65 BK

    Basi Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen.

  18. 1 Timotheo 1:18takriban 65 BK

    Mwanangu Timotheo, ninakupa agizo hili, kwa kadiri ya maneno ya unabii yaliyosemwa kukuhusu, ili kwa kuyafuata upate kupigana vita vizuri,

  19. 1 Timotheo 1:19takriban 65 BK

    ukiishikilia imani na dhamiri njema, ambazo wengine wamevikataa, na hivyo wakaangamia kwa habari ya imani yao.

  20. 1 Timotheo 1:20takriban 65 BK

    Miongoni mwao wako Himenayo na Aleksanda, ambao nimemkabidhi Shetani ili wafundishwe wasije wakakufuru.

  21. 1 Timotheo 2:1takriban 65 BK

    Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote:

  22. 1 Timotheo 2:2takriban 65 BK

    kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu.

  23. 1 Timotheo 2:3takriban 65 BK

    Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu,

  24. 1 Timotheo 2:4takriban 65 BK

    anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli.

  25. 1 Timotheo 2:5takriban 65 BK

    Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu,