Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yakobo 1:1takriban 60 BK

    Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo: Kwa makabila kumi na mawili yaliyotawanyika ulimwenguni: Salamu.

  2. Yakobo 1:2takriban 60 BK

    Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali,

  3. Yakobo 1:3takriban 60 BK

    kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

  4. Yakobo 1:4takriban 60 BK

    Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote.

  5. Yakobo 1:5takriban 60 BK

    Kama mtu yeyote miongoni mwenu amepungukiwa na hekima na amwombe Mungu, yeye awapaye watu wote kwa ukarimu wala hana kinyongo, naye atapewa.

  6. Yakobo 1:6takriban 60 BK

    Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, lililochukuliwa na upepo na kutupwa huku na huku.

  7. Yakobo 1:7takriban 60 BK

    Mtu kama huyo asidhani ya kuwa atapata kitu chochote kutoka kwa Bwana.

  8. Yakobo 1:8takriban 60 BK

    Yeye ni mtu mwenye nia mbili, mwenye kusitasita katika njia zake zote.

  9. Yakobo 1:9takriban 60 BK

    Ndugu asiye na cheo kikubwa yampasa ajivunie hali hiyo maana ametukuzwa.

  10. Yakobo 1:10takriban 60 BK

    Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani.

  11. Yakobo 1:11takriban 60 BK

    Kwa maana jua kali lenye kuchoma huchomoza na kuliunguza, likayakausha majani, na ua lake likapukutika, nao uzuri wake huharibika. Vivyo hivyo tajiri naye atanyauka akiwa anaendelea na shughuli zake.

  12. Yakobo 1:12takriban 60 BK

    Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mungu alilowaahidia wale wampendao.

  13. Yakobo 1:13takriban 60 BK

    Mtu anapojaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu.” Kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye hamjaribu mtu yeyote.

  14. Yakobo 1:14takriban 60 BK

    Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya.

  15. Yakobo 1:15takriban 60 BK

    Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti.

  16. Yakobo 1:16takriban 60 BK

    Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike.

  17. Yakobo 1:17takriban 60 BK

    Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.

  18. Yakobo 1:18takriban 60 BK

    Kwa mapenzi yake mwenyewe alituzaa kwa neno la kweli, kusudi tuwe kama mazao ya kwanza katika viumbe vyake vyote.

  19. Yakobo 1:19takriban 60 BK

    Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika.

  20. Yakobo 1:20takriban 60 BK

    Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu.

  21. Yakobo 1:21takriban 60 BK

    Kwa hiyo, ondoleeni mbali uchafu wote na uovu ambao umezidi kuwa mwingi, mkalipokee kwa unyenyekevu lile Neno lililopandwa ndani yenu ambalo laweza kuokoa nafsi zenu.

  22. Yakobo 1:22takriban 60 BK

    Basi kuweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu.

  23. Yakobo 1:23takriban 60 BK

    Kwa maana kama mtu ni msikiaji tu wa Neno wala hatendi kile linachosema, yeye ni kama mtu ajitazamaye uso wake kwenye kioo

  24. Yakobo 1:24takriban 60 BK

    na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara husahau jinsi alivyo.

  25. Yakobo 1:25takriban 60 BK

    Lakini yeye anayeangalia kwa bidii katika sheria kamilifu, ile iletayo uhuru, naye akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosikia, bali akalitenda, atabarikiwa katika kile anachofanya.