Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Yohana 1:1takriban 90 BK

    Tunawajulisha lile lililokuwepo tangu mwanzo, lile tulilosikia, ambalo tumeliona kwa macho yetu, ambalo tumelitazama na kuligusa kwa mikono yetu, kuhusu Neno la uzima.

  2. 1 Yohana 1:2takriban 90 BK

    Uzima huo ulidhihirishwa; nasi tumeuona na kuushuhudia, nasi twawatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa pamoja na Baba, nao ukadhihirishwa kwetu.

  3. 1 Yohana 1:3takriban 90 BK

    Twawatangazia lile tuliloliona na kulisikia, ili nanyi mwe na ushirika nasi. Na ushirika wetu hasa ni pamoja na Baba na Mwanawe, Yesu Kristo.

  4. 1 Yohana 1:4takriban 90 BK

    Tunaandika mambo haya ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.

  5. 1 Yohana 1:5takriban 90 BK

    Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote.

  6. 1 Yohana 1:6takriban 90 BK

    Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli.

  7. 1 Yohana 1:7takriban 90 BK

    Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

  8. 1 Yohana 1:8takriban 90 BK

    Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu.

  9. 1 Yohana 1:9takriban 90 BK

    Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.

  10. 1 Yohana 1:10takriban 90 BK

    Kama tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo na neno lake halimo ndani yetu.

  11. 1 Yohana 2:1takriban 90 BK

    Watoto wangu wapendwa, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba: ndiye Yesu Kristo, Mwenye Haki.

  12. 1 Yohana 2:2takriban 90 BK

    Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote.

  13. 1 Yohana 2:3takriban 90 BK

    Basi katika hili twajua ya kuwa tumemjua, tukizishika amri zake.

  14. 1 Yohana 2:4takriban 90 BK

    Mtu yeyote asemaye kuwa, “Ninamjua,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, wala ndani ya mtu huyo hamna kweli.

  15. 1 Yohana 2:5takriban 90 BK

    Lakini mtu yeyote anayelitii neno lake, upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kweli kweli. Katika hili twajua kuwa tumo ndani yake.

  16. 1 Yohana 2:6takriban 90 BK

    Yeyote anayesema anakaa ndani yake hana budi kuenenda kama Yesu alivyoenenda.

  17. 1 Yohana 2:7takriban 90 BK

    Wapendwa, siwaandikii ninyi amri mpya bali ile ya zamani, ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilosikia.

  18. 1 Yohana 2:8takriban 90 BK

    Lakini nawaandikia amri mpya, yaani, lile neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli tayari inangʼaa.

  19. 1 Yohana 2:9takriban 90 BK

    Yeyote anayesema yumo nuruni lakini anamchukia ndugu yake bado yuko gizani.

  20. 1 Yohana 2:10takriban 90 BK

    Yeye ampendaye ndugu yake anakaa nuruni, wala hakuna kitu chochote ndani yake cha kumkwaza.

  21. 1 Yohana 2:11takriban 90 BK

    Lakini yeyote amchukiaye ndugu yake, yuko gizani na anaenenda gizani, wala hajui anakokwenda, kwa sababu giza limempofusha macho.

  22. 1 Yohana 2:12takriban 90 BK

    Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu dhambi zenu zimesamehewa kwa ajili ya Jina lake.

  23. 1 Yohana 2:13takriban 90 BK

    Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nawaandikia ninyi watoto wadogo, kwa sababu mmemjua Baba.

  24. 1 Yohana 2:14takriban 90 BK

    Nawaandikia ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

  25. 1 Yohana 2:15takriban 90 BK

    Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake.