Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Wagalatia 1:1takriban 58 BK

    Paulo mtume: si mtume wa wanadamu wala aliyetumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu;

  2. Wagalatia 1:2takriban 58 BK

    na ndugu wote walio pamoja nami: Kwa makanisa ya Galatia:

  3. Wagalatia 1:3takriban 58 BK

    Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo,

  4. Wagalatia 1:4takriban 58 BK

    aliyejitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu wa sasa ulio mbaya, sawasawa na mapenzi yake yeye aliye Mungu na Baba yetu.

  5. Wagalatia 1:5takriban 58 BK

    Utukufu una yeye milele na milele. Amen.

  6. Wagalatia 1:6takriban 58 BK

    Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata Injili nyingine,

  7. Wagalatia 1:7takriban 58 BK

    ambayo kwa kweli si Injili kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya na wanaotaka kuipotosha Injili ya Kristo.

  8. Wagalatia 1:8takriban 58 BK

    Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri Injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo alaaniwe milele!

  9. Wagalatia 1:9takriban 58 BK

    Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu yeyote atawahubiria Injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!

  10. Wagalatia 1:10takriban 58 BK

    Je, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Kristo.

  11. Wagalatia 1:11takriban 58 BK

    Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu.

  12. Wagalatia 1:12takriban 58 BK

    Kwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo.

  13. Wagalatia 1:13takriban 58 BK

    Ninyi mmekwisha kusikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kwa nguvu na kujaribu kuliangamiza.

  14. Wagalatia 1:14takriban 58 BK

    Nami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika yangu maana nilijitahidi sana katika desturi za baba zangu.

  15. Wagalatia 1:15takriban 58 BK

    Lakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake,

  16. Wagalatia 1:16takriban 58 BK

    alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote,

  17. Wagalatia 1:17takriban 58 BK

    wala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.

  18. Wagalatia 1:18takriban 58 BK

    Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kuonana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano.

  19. Wagalatia 1:19takriban 58 BK

    Lakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana.

  20. Wagalatia 1:20takriban 58 BK

    Nawahakikishia mbele za Mungu kuwa ninayowaandikia si uongo.

  21. Wagalatia 1:21takriban 58 BK

    Baadaye nilikwenda sehemu za Syria na Kilikia.

  22. Wagalatia 1:22takriban 58 BK

    Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa makanisa ya huko Uyahudi yaliyo katika Kristo.

  23. Wagalatia 1:23takriban 58 BK

    Wao walisikia habari tu kwamba, “Mtu yule ambaye hapo kwanza alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akijaribu kuiangamiza.”

  24. Wagalatia 1:24takriban 58 BK

    Nao wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.

  25. Wagalatia 2:1takriban 52 BK

    Kisha, baada ya miaka kumi na minne, nilipanda tena kwenda Yerusalemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito ili awe pamoja nami.