- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa AD 48–96
Letters to the Churches
Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.
Mistari ya kipindi hiki
- 1 Wakorintho 12:22takriban 59 BK
Lakini badala yake, vile viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa dhaifu, ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana.
- 1 Wakorintho 12:23takriban 59 BK
Navyo vile viungo tunavyoviona havina heshima, ndivyo tunavipa heshima maalum. Vile viungo vya mwili ambavyo havina uzuri, tunavipa heshima ya pekee;
- 1 Wakorintho 12:24takriban 59 BK
wakati vile viungo vyenye uzuri havihitaji utunzaji wa pekee. Lakini Mungu ameviweka pamoja viungo vya mwili na akavipa heshima zaidi vile vilivyopungukiwa,
- 1 Wakorintho 12:25takriban 59 BK
ili pasiwe na mafarakano katika mwili, bali viungo vyote vihudumiane kwa usawa kila kimoja na mwenzake.
- 1 Wakorintho 12:26takriban 59 BK
Kama kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia pamoja nacho, kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
- 1 Wakorintho 12:27takriban 59 BK
Sasa ninyi ni mwili wa Kristo na kila mmoja wenu ni sehemu ya huo mwili.
- 1 Wakorintho 12:28takriban 59 BK
Mungu ameweka katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, pia karama za kuponya, karama za kusaidiana, karama za uongozi, aina mbalimbali za lugha.
- 1 Wakorintho 12:29takriban 59 BK
Je, wote ni mitume? Je, wote ni manabii? Je, wote ni walimu? Je, wote wanatenda miujiza?
- 1 Wakorintho 12:30takriban 59 BK
Je, wote wana karama ya kuponya? Je, wote hunena kwa lugha mpya? Je, wote wanatafsiri?
- 1 Wakorintho 12:31takriban 59 BK
Basi tamanini sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonyesha njia iliyo bora zaidi.
- 1 Wakorintho 13:1takriban 59 BK
Hata kama nitasema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolialia au toazi livumalo.
- 1 Wakorintho 13:2takriban 59 BK
Ningekuwa na karama ya unabii na kujua siri zote na maarifa yote, hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.
- 1 Wakorintho 13:3takriban 59 BK
Kama nikitoa mali yote niliyo nayo na kama nikijitolea mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.
- 1 Wakorintho 13:4takriban 59 BK
Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi.
- 1 Wakorintho 13:5takriban 59 BK
Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.
- 1 Wakorintho 13:6takriban 59 BK
Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli.
- 1 Wakorintho 13:7takriban 59 BK
Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.
- 1 Wakorintho 13:8takriban 59 BK
Upendo haushindwi kamwe. Lakini ukiwepo unabii, utakoma; zikiwepo lugha, zitakoma; yakiwepo maarifa, yatapita.
- 1 Wakorintho 13:9takriban 59 BK
Kwa maana tunafahamu kwa sehemu na tunatoa unabii kwa sehemu.
- 1 Wakorintho 13:10takriban 59 BK
Lakini ukamilifu ukija, yale yasiyo kamili hutoweka.
- 1 Wakorintho 13:11takriban 59 BK
Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, niliwaza kama mtoto, nilifikiri kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto.
- 1 Wakorintho 13:12takriban 59 BK
Kwa maana sasa tunaona taswira kama kwa kioo, lakini wakati huo tutaona wazi. Sasa nafahamu kwa sehemu, wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile mimi ninavyofahamika kikamilifu.
- 1 Wakorintho 13:13takriban 59 BK
Basi sasa, yanadumu mambo haya matatu: Imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu miongoni mwa haya matatu ni upendo.
- 1 Wakorintho 14:1takriban 59 BK
Fuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii.
- 1 Wakorintho 14:2takriban 59 BK
Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho.