- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa AD 48–96
Letters to the Churches
Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.
Mistari ya kipindi hiki
- 1 Wakorintho 14:28takriban 59 BK
Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu.
- 1 Wakorintho 14:29takriban 59 BK
Manabii wawili au watatu wanene na wengine wapime yale yasemwayo.
- 1 Wakorintho 14:30takriban 59 BK
Kama mtu yeyote aliyeketi karibu, akipata ufunuo, basi yule wa kwanza na anyamaze.
- 1 Wakorintho 14:31takriban 59 BK
Kwa maana wote mnaweza kutoa unabii, mmoja baada ya mwingine, ili kila mtu apate kufundishwa na kutiwa moyo.
- 1 Wakorintho 14:32takriban 59 BK
Roho za manabii huwatii manabii.
- 1 Wakorintho 14:33takriban 59 BK
Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani. Kama ilivyo katika makusanyiko yote ya watakatifu,
- 1 Wakorintho 14:34takriban 59 BK
wanawake wanapaswa kuwa kimya kanisani. Hawaruhusiwi kusema, bali wanyenyekee kama sheria isemavyo.
- 1 Wakorintho 14:35takriban 59 BK
Kama wakitaka kuuliza kuhusu jambo lolote, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza kanisani.
- 1 Wakorintho 14:36takriban 59 BK
Je, neno la Mungu lilianzia kwenu? Au ni ninyi tu ambao neno la Mungu limewafikia?
- 1 Wakorintho 14:37takriban 59 BK
Kama mtu yeyote akidhani kwamba yeye ni nabii, au ana karama za rohoni, basi na akubali kwamba haya ninayoandika ni maagizo kutoka kwa Bwana.
- 1 Wakorintho 14:38takriban 59 BK
Kama mtu akipuuza jambo hili yeye mwenyewe atapuuzwa.
- 1 Wakorintho 14:39takriban 59 BK
Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha.
- 1 Wakorintho 14:40takriban 59 BK
Lakini kila kitu kitendeke kwa heshima na kwa utaratibu.
- 1 Wakorintho 15:1takriban 59 BK
Basi ndugu zangu nataka niwakumbushe kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo katika hiyo mmesimama.
- 1 Wakorintho 15:2takriban 59 BK
Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.
- 1 Wakorintho 15:3takriban 59 BK
Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko,
- 1 Wakorintho 15:4takriban 59 BK
ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko,
- 1 Wakorintho 15:5takriban 59 BK
na kwamba alimtokea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili.
- 1 Wakorintho 15:6takriban 59 BK
Baadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala.
- 1 Wakorintho 15:7takriban 59 BK
Ndipo akamtokea Yakobo na kisha mitume wote.
- 1 Wakorintho 15:8takriban 59 BK
Mwisho wa wote, akanitokea mimi pia, ambaye ni kama aliyezaliwa si kwa wakati wake.
- 1 Wakorintho 15:9takriban 59 BK
Kwa maana mimi ndiye mdogo kuliko mitume wote, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu.
- 1 Wakorintho 15:10takriban 59 BK
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote, lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami.
- 1 Wakorintho 15:11takriban 59 BK
Hivyo basi, kama ilikuwa mimi au wao, hili ndilo tunalohubiri, na hili ndilo mliloamini.
- 1 Wakorintho 15:12takriban 59 BK
Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu?