Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Wakorintho 15:13takriban 59 BK

    Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo hakufufuliwa.

  2. 1 Wakorintho 15:14takriban 59 BK

    Tena ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, kuhubiri kwetu kumekuwa ni bure na imani yenu ni batili.

  3. 1 Wakorintho 15:15takriban 59 BK

    Zaidi ya hayo, twaonekana kuwa mashahidi wa uongo kuhusu Mungu, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu kwamba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu, lakini hilo haliwezi kuwa kweli kama wafu hawafufuliwi.

  4. 1 Wakorintho 15:16takriban 59 BK

    Kwa kuwa kama wafu hawafufuliwi, basi hata Kristo hajafufuka.

  5. 1 Wakorintho 15:17takriban 59 BK

    Tena kama Kristo hajafufuliwa, imani yenu ni batili; nanyi bado mko katika dhambi zenu.

  6. 1 Wakorintho 15:18takriban 59 BK

    Hivyo basi, wote waliolala katika Kristo wamepotea.

  7. 1 Wakorintho 15:19takriban 59 BK

    Ikiwa tumaini letu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wote.

  8. 1 Wakorintho 15:20takriban 59 BK

    Lakini kweli Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, tunda la kwanza la wale wote waliolala.

  9. 1 Wakorintho 15:21takriban 59 BK

    Kwa maana kama vile mauti ilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja.

  10. 1 Wakorintho 15:22takriban 59 BK

    Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai.

  11. 1 Wakorintho 15:23takriban 59 BK

    Lakini kila mmoja kwa wakati wake: Kristo, tunda la kwanza kisha, wale walio wake, wakati atakapokuja.

  12. 1 Wakorintho 15:24takriban 59 BK

    Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu.

  13. 1 Wakorintho 15:25takriban 59 BK

    Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake.

  14. 1 Wakorintho 15:26takriban 59 BK

    Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni mauti.

  15. 1 Wakorintho 15:27takriban 59 BK

    Kwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Kristo hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa.

  16. 1 Wakorintho 15:28takriban 59 BK

    Atakapokuwa amekwisha kuyafanya haya, ndipo Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aliyetiisha vitu vyote, ili Mungu awe yote katika yote.

  17. 1 Wakorintho 15:29takriban 59 BK

    Basi kama hakuna ufufuo, watafanyaje wale wabatizwao kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa ajili yao?

  18. 1 Wakorintho 15:30takriban 59 BK

    Nasi kwa upande wetu kwa nini tunajihatarisha kila saa?

  19. 1 Wakorintho 15:31takriban 59 BK

    Kama majivuno yangu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu ni kweli, ndugu zangu, ninakufa kila siku.

  20. 1 Wakorintho 15:32takriban 59 BK

    Kama kwa sababu za kibinadamu tu nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, ningekuwa nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi, “Tuleni na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa.”

  21. 1 Wakorintho 15:33takriban 59 BK

    Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.”

  22. 1 Wakorintho 15:34takriban 59 BK

    Zindukeni mwe na akili kama iwapasavyo, wala msitende dhambi tena; kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya ili mwone aibu.

  23. 1 Wakorintho 15:35takriban 59 BK

    Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?”

  24. 1 Wakorintho 15:36takriban 59 BK

    Ninyi wapumbavu kiasi gani? Mpandacho hakiwi hai kama hakikufa.

  25. 1 Wakorintho 15:37takriban 59 BK

    Mpandapo, hampandi mwili ule utakao kuwa, bali mwapanda mbegu tu, pengine ya ngano au ya kitu kingine.