Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Wakorintho 15:38takriban 59 BK

    Lakini Mungu huipa mbegu umbo kama alivyokusudia mwenyewe na kila aina ya mbegu huipa umbo lake.

  2. 1 Wakorintho 15:39takriban 59 BK

    Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine, kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti.

  3. 1 Wakorintho 15:40takriban 59 BK

    Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani, lakini fahari wa ile miili ya mbinguni ni wa aina moja na fahari wa ile miili ya duniani ni wa aina nyingine.

  4. 1 Wakorintho 15:41takriban 59 BK

    Jua lina fahari ya aina moja, mwezi nao una fahari yake na nyota pia, nazo nyota hutofautiana katika fahari.

  5. 1 Wakorintho 15:42takriban 59 BK

    Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Ule mwili wa kuharibika uliopandwa, utafufuliwa usioharibika,

  6. 1 Wakorintho 15:43takriban 59 BK

    unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu, unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu,

  7. 1 Wakorintho 15:44takriban 59 BK

    unapandwa mwili wa asili, unafufuliwa mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia.

  8. 1 Wakorintho 15:45takriban 59 BK

    Kwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai”; Adamu wa mwisho, yeye ni roho iletayo uzima.

  9. 1 Wakorintho 15:46takriban 59 BK

    Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho.

  10. 1 Wakorintho 15:47takriban 59 BK

    Mtu wa kwanza aliumbwa kwa mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni.

  11. 1 Wakorintho 15:48takriban 59 BK

    Kama vile alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na kwa vile alivyo mtu yule aliyetoka mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni.

  12. 1 Wakorintho 15:49takriban 59 BK

    Kama vile tulivyochukua mfano wa mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua mfano wa yule mtu aliyetoka mbinguni.

  13. 1 Wakorintho 15:50takriban 59 BK

    Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika.

  14. 1 Wakorintho 15:51takriban 59 BK

    Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa

  15. 1 Wakorintho 15:52takriban 59 BK

    ghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa.

  16. 1 Wakorintho 15:53takriban 59 BK

    Kwa maana mwili huu wa kuharibika lazima uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa lazima uvae kutokufa.

  17. 1 Wakorintho 15:54takriban 59 BK

    Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”

  18. 1 Wakorintho 15:55takriban 59 BK

    “Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako? Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?”

  19. 1 Wakorintho 15:56takriban 59 BK

    Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria.

  20. 1 Wakorintho 15:57takriban 59 BK

    Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

  21. 1 Wakorintho 15:58takriban 59 BK

    Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure.

  22. 1 Wakorintho 16:1takriban 59 BK

    Basi kuhusu changizo kwa ajili ya watakatifu: Kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo.

  23. 1 Wakorintho 16:2takriban 59 BK

    Siku ya kwanza ya kila juma, kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha, kulingana na mapato yake na fedha hizo aziweke akiba, ili nitakapokuja pasiwe na lazima ya kufanya mchango.

  24. 1 Wakorintho 16:3takriban 59 BK

    Kwa hiyo nitakapowasili, nitawapa wale mtakaowachagua barua za kuwatambulisha, ili kuwatuma wapeleke zawadi zenu huko Yerusalemu.

  25. 1 Wakorintho 16:4takriban 59 BK

    Kama ikionekana ni vyema na mimi niende, basi hao watu watafuatana nami.