Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Wakorintho 16:5takriban 59 BK

    Baada ya kupitia Makedonia nitakuja kwenu, maana ninakusudia kupitia Makedonia.

  2. 1 Wakorintho 16:6takriban 59 BK

    Huenda nitakaa nanyi kwa muda, au hata kukaa nanyi kipindi chote cha baridi, ili mweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendapo.

  3. 1 Wakorintho 16:7takriban 59 BK

    Kwa maana sitaki niwaone sasa na kupita tu; natarajia kuwa nanyi kwa muda wa kutosha, kama Bwana akipenda.

  4. 1 Wakorintho 16:8takriban 59 BK

    Lakini nitakaa Efeso mpaka wakati wa Pentekoste,

  5. 1 Wakorintho 16:9takriban 59 BK

    kwa maana mlango mkubwa umefunguliwa kwangu kufanya kazi yenye matunda, nako huko kuna adui wengi wanaonipinga.

  6. 1 Wakorintho 16:10takriban 59 BK

    Ikiwa Timotheo atakuja kwenu, hakikisheni kwamba hana hofu yoyote akiwa nanyi, kwa sababu anafanya kazi ya Bwana, kama mimi nifanyavyo.

  7. 1 Wakorintho 16:11takriban 59 BK

    Basi asiwepo mtu atakayekataa kumpokea. Msafirisheni kwa amani ili aweze kunijia tena. Namtarajia pamoja na ndugu.

  8. 1 Wakorintho 16:12takriban 59 BK

    Basi kwa habari za ndugu yetu Apolo, nimemsihi kwa bidii aje kwenu pamoja na hao ndugu. Ingawa alikuwa hapendi kabisa kuja sasa, lakini atakuja apatapo nafasi.

  9. 1 Wakorintho 16:13takriban 59 BK

    Kesheni, simameni imara katika imani, fanyeni kiume, kuweni mashujaa kuweni hodari.

  10. 1 Wakorintho 16:14takriban 59 BK

    Fanyeni kila kitu katika upendo.

  11. 1 Wakorintho 16:15takriban 59 BK

    Ninyi mnajua kwamba watu wa nyumbani mwa Stefana ndio waliokuwa wa kwanza kuamini katika Akaya, nao wamejitoa kwa ajili ya kuwahudumia watakatifu. Ndugu nawasihi,

  12. 1 Wakorintho 16:16takriban 59 BK

    mjitie katika kuwahudumia watu kama hawa na kila mmoja aingiaye kwenye kazi na kuifanya kwa bidii.

  13. 1 Wakorintho 16:17takriban 59 BK

    Nilifurahi wakati Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa sababu wamenipatia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu.

  14. 1 Wakorintho 16:18takriban 59 BK

    Kwa kuwa waliiburudisha roho yangu na zenu pia. Watu kama hawa wanastahili kutambuliwa.

  15. 1 Wakorintho 16:19takriban 59 BK

    Makanisa ya Asia yanawasalimu. Akila na Prisila, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao wanawasalimu sana katika Bwana.

  16. 1 Wakorintho 16:20takriban 59 BK

    Ndugu wote walioko hapa wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.

  17. 1 Wakorintho 16:21takriban 59 BK

    Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe.

  18. 1 Wakorintho 16:22takriban 59 BK

    Kama mtu yeyote hampendi Bwana Yesu Kristo, na alaaniwe. Bwana wetu, njoo.

  19. 1 Wakorintho 16:23takriban 59 BK

    Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.

  20. 1 Wakorintho 16:24takriban 59 BK

    Upendo wangu uwe nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amen.

  21. 2 Wakorintho 1:1takriban 60 BK

    Barua hii ni kutoka kwangu mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu, Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko Akaya yote:

  22. 2 Wakorintho 1:2takriban 60 BK

    Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.

  23. 2 Wakorintho 1:3takriban 60 BK

    Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote.

  24. 2 Wakorintho 1:4takriban 60 BK

    Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.

  25. 2 Wakorintho 1:5takriban 60 BK

    Kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi ndani ya maisha yetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kwa njia ya Kristo.