Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Wakorintho 2:7takriban 60 BK

    Basi sasa badala yake, inawapasa kumsamehe na kumfariji, ili asigubikwe na huzuni kupita kiasi.

  2. 2 Wakorintho 2:8takriban 60 BK

    Kwa hiyo, nawasihi, mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwa ajili yake.

  3. 2 Wakorintho 2:9takriban 60 BK

    Sababu ya kuwaandikia ni kuona kama mngeweza kushinda hilo jaribio na kutii katika kila jambo.

  4. 2 Wakorintho 2:10takriban 60 BK

    Kama ninyi mkimsamehe mtu yeyote, mimi pia nimemsamehe. Kile nilichosamehe, kama kulikuwa na kitu chochote cha kusamehe, nimekwisha kusamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu,

  5. 2 Wakorintho 2:11takriban 60 BK

    ili Shetani asitushinde. Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake.

  6. 2 Wakorintho 2:12takriban 60 BK

    Basi nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Kristo na kukuta kwamba Bwana alikuwa amenifungulia mlango,

  7. 2 Wakorintho 2:13takriban 60 BK

    bado nilikuwa sina utulivu akilini mwangu kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Hivyo niliagana nao nikaenda Makedonia.

  8. 2 Wakorintho 2:14takriban 60 BK

    Lakini Mungu ashukuriwe, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye.

  9. 2 Wakorintho 2:15takriban 60 BK

    Kwa maana sisi kwa Mungu ni harufu nzuri ya manukato ya Kristo miongoni mwa wale wanaookolewa na kwa wale wanaopotea.

  10. 2 Wakorintho 2:16takriban 60 BK

    Kwa wale wanaopotea, sisi ni harufu ya mauti iletayo mauti; lakini kwa wale wanaookolewa, sisi ni harufu nzuri iletayo uzima. Ni nani awezaye mambo hayo?

  11. 2 Wakorintho 2:17takriban 60 BK

    Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatufanyi biashara na Neno la Mungu kwa ajili ya kupata faida. Kinyume chake, katika Kristo tunalisema Neno la Mungu kwa unyoofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa Mungu.

  12. 2 Wakorintho 3:1takriban 60 BK

    Je, tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine?

  13. 2 Wakorintho 3:2takriban 60 BK

    Ninyi wenyewe ndio barua yetu iliyoandikwa katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na kila mtu.

  14. 2 Wakorintho 3:3takriban 60 BK

    Nanyi mwadhihirisha wazi kwamba ninyi ni barua itokayo kwa Kristo, matokeo ya huduma yetu, ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni mioyo ya wanadamu.

  15. 2 Wakorintho 3:4takriban 60 BK

    Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo.

  16. 2 Wakorintho 3:5takriban 60 BK

    Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lolote wenyewe, lakini nguvu yetu inatoka kwa Mungu.

  17. 2 Wakorintho 3:6takriban 60 BK

    Ndiye alituwezesha sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima.

  18. 2 Wakorintho 3:7takriban 60 BK

    Basi ikiwa ile huduma iliyoleta mauti, iliyoandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu, hata Waisraeli wakawa hawawezi kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya ule utukufu wake ingawa ulikuwa ni wa kufifia,

  19. 2 Wakorintho 3:8takriban 60 BK

    je, huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi?

  20. 2 Wakorintho 3:9takriban 60 BK

    Ikiwa huduma ile inayowahukumu wanadamu ina utukufu, je, ile huduma iletayo haki haitakuwa ya utukufu zaidi?

  21. 2 Wakorintho 3:10takriban 60 BK

    Kwa maana kile kilichokuwa na utukufu sasa hakina utukufu ukilinganisha na huu utukufu unaozidi wa Agano Jipya.

  22. 2 Wakorintho 3:11takriban 60 BK

    Ikiwa kile kilichokuwa kinafifia kilikuja kwa utukufu, je, si zaidi utukufu wa kile kinachodumu?

  23. 2 Wakorintho 3:12takriban 60 BK

    Kwa hiyo, kwa kuwa tunalo tumaini hili, tuna ujasiri sana.

  24. 2 Wakorintho 3:13takriban 60 BK

    Sisi si kama Mose, ambaye ilimpasa kuweka utaji ili kufunika uso wake ili Waisraeli wasiuone ule mngʼao uliokuwa juu yake hadi ulipofifia na hatimaye kutoweka.

  25. 2 Wakorintho 3:14takriban 60 BK

    Lakini akili zao zilipumbazwa, kwa maana mpaka leo utaji ule ule hufunika wakati Agano la Kale linasomwa. Huo utaji haujaondolewa, kwa maana ni katika Kristo peke yake unaondolewa.