- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
Creation Era
The Tower of Babel
Scattered nations and confused languages mark the beginning of the diversity of peoples across the earth.
Mistari ya kipindi hiki
- Mwanzo 10:26takriban 2247 KK
Yoktani alikuwa baba wa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
- Mwanzo 10:27takriban 2247 KK
Hadoramu, Uzali, Dikla,
- Mwanzo 10:28takriban 2207 KK
Obali, Abimaeli, Sheba,
- Mwanzo 10:29takriban 2207 KK
Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
- Mwanzo 10:30takriban 2207 KK
Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.
- Mwanzo 10:31takriban 2207 KK
Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
- Mwanzo 10:32takriban 2207 KK
Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.
- Mwanzo 11:1takriban 2247 KK
Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja.
- Mwanzo 11:2takriban 2247 KK
Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari nao wakaishi huko.
- Mwanzo 11:3takriban 2247 KK
Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali.
- Mwanzo 11:4takriban 2247 KK
Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.”
- Mwanzo 11:5takriban 2247 KK
Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga.
- Mwanzo 11:6takriban 2247 KK
Bwana akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao.
- Mwanzo 11:7takriban 2247 KK
Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”
- Mwanzo 11:8takriban 2247 KK
Hivyo Bwana akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji.
- Mwanzo 11:9takriban 2247 KK
Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote.
- Mwanzo 11:10takriban 2346 KK
Hivi ndivyo vizazi vya Shemu. Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi.
- Mwanzo 11:11takriban 1846 KK
Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.
- Mwanzo 11:12takriban 2311 KK
Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela.
- Mwanzo 11:13takriban 1908 KK
Baada ya Arfaksadi kumzaa Shela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.
- Mwanzo 11:14takriban 2281 KK
Shela alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Eberi.
- Mwanzo 11:15takriban 1878 KK
Shela baada ya kumzaa Eberi, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.
- Mwanzo 11:16takriban 2247 KK
Eberi alipokuwa na miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.
- Mwanzo 11:17takriban 1817 KK
Baada ya Eberi kumzaa Pelegi, aliishi miaka 430, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.
- Mwanzo 11:18takriban 2217 KK
Pelegi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Reu.