Skip to content

Shem

17 mistari · 8 wanafamilia

Anajulikana pia kama: Sem

Mistari inayomtaja Shem

  1. Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.

  2. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.

  3. Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina.

  4. Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.)

  5. Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

  6. Pia akasema, “Abarikiwe Bwana, Mungu wa Shemu! Kanaani na awe mtumwa wa Shemu.

  7. Mungu na apanue mipaka ya Yafethi; Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu, na Kanaani na awe mtumwa wake.”

  8. Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

  9. Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

  10. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

  11. Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

  12. Hivi ndivyo vizazi vya Shemu. Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi.

  13. Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

  14. Wana wa Noa walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi.

  15. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

  16. Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,

  17. Sala alikuwa mwana wa Kenani, Kenani alikuwa mwana wa Arfaksadi, Arfaksadi alikuwa mwana wa Shemu, Shemu alikuwa mwana wa Noa, Noa alikuwa mwana wa Lameki,