Skip to content

Creation Era

Creation & The Fall

God creates the heavens and earth, forming humanity in his image before sin enters the world.

138 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 1:1takriban 4004 KK

    Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia.

  2. Mwanzo 1:2takriban 4004 KK

    Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

  3. Mwanzo 1:3takriban 4004 KK

    Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo.

  4. Mwanzo 1:4takriban 4004 KK

    Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza.

  5. Mwanzo 1:5takriban 4004 KK

    Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

  6. Mwanzo 1:6takriban 4004 KK

    Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.”

  7. Mwanzo 1:7takriban 4004 KK

    Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo.

  8. Mwanzo 1:8takriban 4004 KK

    Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.

  9. Mwanzo 1:9takriban 4004 KK

    Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo.

  10. Mwanzo 1:10takriban 4004 KK

    Mungu akaiita nchi kavu “ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.

  11. Mwanzo 1:11takriban 4004 KK

    Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo.

  12. Mwanzo 1:12takriban 4004 KK

    Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema.

  13. Mwanzo 1:13takriban 4004 KK

    Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu.

  14. Mwanzo 1:14takriban 4004 KK

    Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka,

  15. Mwanzo 1:15takriban 4004 KK

    nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo.

  16. Mwanzo 1:16takriban 4004 KK

    Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota.

  17. Mwanzo 1:17takriban 4004 KK

    Mungu akaiweka katika nafasi ya anga iangaze dunia,

  18. Mwanzo 1:18takriban 4004 KK

    itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

  19. Mwanzo 1:19takriban 4004 KK

    Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya nne.

  20. Mwanzo 1:20takriban 4004 KK

    Mungu akasema, “Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga.”

  21. Mwanzo 1:21takriban 4004 KK

    Kwa hiyo Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

  22. Mwanzo 1:22takriban 4004 KK

    Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia.”

  23. Mwanzo 1:23takriban 4004 KK

    Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano.

  24. Mwanzo 1:24takriban 4004 KK

    Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo.

  25. Mwanzo 1:25takriban 4004 KK

    Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.