Rukia maudhui

Creation Era

Creation & The Fall

God creates the heavens and earth, forming humanity in his image before sin enters the world.

138 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 2:20takriban 4004 KK

    Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini. Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa.

  2. Mwanzo 2:21takriban 4004 KK

    Hivyo Bwana Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama.

  3. Mwanzo 2:22takriban 4004 KK

    Kisha Bwana Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

  4. Mwanzo 2:23takriban 4004 KK

    Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’ kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”

  5. Mwanzo 2:24takriban 4004 KK

    Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

  6. Mwanzo 2:25takriban 4004 KK

    Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.

  7. Mwanzo 3:1takriban 4004 KK

    Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”

  8. Mwanzo 3:2takriban 4004 KK

    Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini,

  9. Mwanzo 3:3takriban 4004 KK

    lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ”

  10. Mwanzo 3:4takriban 4004 KK

    Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa.

  11. Mwanzo 3:5takriban 4004 KK

    Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

  12. Mwanzo 3:6takriban 4004 KK

    Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala.

  13. Mwanzo 3:7takriban 4004 KK

    Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.

  14. Mwanzo 3:8takriban 4004 KK

    Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani.

  15. Mwanzo 3:9takriban 4004 KK

    Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?”

  16. Mwanzo 3:10takriban 4004 KK

    Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.”

  17. Mwanzo 3:11takriban 4004 KK

    Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”

  18. Mwanzo 3:12takriban 4004 KK

    Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.”

  19. Mwanzo 3:13takriban 4004 KK

    Ndipo Bwana Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.”

  20. Mwanzo 3:14takriban 4004 KK

    Hivyo Bwana Mungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili, “Umelaaniwa kuliko wanyama wote wa kufugwa na wa porini! Utatambaa kwa tumbo lako na kula mavumbi siku zote za maisha yako.

  21. Mwanzo 3:15takriban 4004 KK

    Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, yeye atakuponda kichwa, nawe utamuuma kisigino.”

  22. Mwanzo 3:16takriban 4004 KK

    Kwa mwanamke akasema, “Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto. Tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala.”

  23. Mwanzo 3:17takriban 4004 KK

    Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’ “Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako, kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo siku zote za maisha yako.

  24. Mwanzo 3:18takriban 4004 KK

    Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako, nawe utakula mimea ya shambani.

  25. Mwanzo 3:19takriban 4004 KK

    Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako hadi utakaporudi ardhini, kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo, kwa kuwa wewe u mavumbi na mavumbini wewe utarudi.”