Skip to content

Creation Era

Creation & The Fall

God creates the heavens and earth, forming humanity in his image before sin enters the world.

138 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 3:20takriban 4004 KK

    Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.

  2. Mwanzo 3:21takriban 4004 KK

    Bwana Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

  3. Mwanzo 3:22takriban 4004 KK

    Kisha Bwana Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.”

  4. Mwanzo 3:23takriban 4004 KK

    Hivyo Bwana Mungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa.

  5. Mwanzo 3:24takriban 4004 KK

    Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.

  6. Mwanzo 4:1takriban 4003 KK

    Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada wa Bwana nimemzaa mwanaume.”

  7. Mwanzo 4:2takriban 4003 KK

    Baadaye akamzaa Abeli ndugu yake. Basi Abeli akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima.

  8. Mwanzo 4:3takriban 4003 KK

    Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa Bwana.

  9. Mwanzo 4:4takriban 4003 KK

    Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. Bwana akamkubali Abeli pamoja na sadaka yake,

  10. Mwanzo 4:5takriban 4003 KK

    lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.

  11. Mwanzo 4:6takriban 4003 KK

    Kisha Bwana akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni?

  12. Mwanzo 4:7takriban 4003 KK

    Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.”

  13. Mwanzo 4:8takriban 4003 KK

    Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua.

  14. Mwanzo 4:9takriban 4003 KK

    Kisha Bwana akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?” Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”

  15. Mwanzo 4:10takriban 4003 KK

    Bwana akasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini.

  16. Mwanzo 4:11takriban 4003 KK

    Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako.

  17. Mwanzo 4:12takriban 4003 KK

    Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.”

  18. Mwanzo 4:13takriban 4003 KK

    Kaini akamwambia Bwana, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili.

  19. Mwanzo 4:14takriban 4003 KK

    Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.”

  20. Mwanzo 4:15takriban 4003 KK

    Lakini Bwana akamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” Kisha Bwana akamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue.

  21. Mwanzo 4:16takriban 4003 KK

    Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za Bwana akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni.

  22. Mwanzo 4:17takriban 4003 KK

    Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Enoki. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Enoki jina la mtoto wake.

  23. Mwanzo 4:18takriban 4003 KK

    Enoki akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli, Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki.

  24. Mwanzo 4:19takriban 4003 KK

    Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila.

  25. Mwanzo 4:20takriban 4003 KK

    Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama.