Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Shem

81 mistari · 4 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.

  2. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.

  3. Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina.

  4. Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.)

  5. Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

  6. Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea,

  7. akasema, “Alaaniwe Kanaani! Atakuwa mtumwa wa chini sana kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.”

  8. Pia akasema, “Abarikiwe Bwana, Mungu wa Shemu! Kanaani na awe mtumwa wa Shemu.

  9. Mungu na apanue mipaka ya Yafethi; Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu, na Kanaani na awe mtumwa wake.”

  10. Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

  11. Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

  12. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

  13. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

  14. Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, naye Shela akamzaa Eberi.

  15. Eberi akapata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

  16. Yoktani alikuwa baba wa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,

  17. Hadoramu, Uzali, Dikla,

  18. Obali, Abimaeli, Sheba,

  19. Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.

  20. Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.

  21. Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

  22. Hivi ndivyo vizazi vya Shemu. Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi.

  23. Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

  24. Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela.

  25. Baada ya Arfaksadi kumzaa Shela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.