Skip to content

Creation Era

The Tower of Babel

Scattered nations and confused languages mark the beginning of the diversity of peoples across the earth.

64 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

  2. Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

  3. Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

  4. Mwanzo 10:4takriban 2338 KK

    Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

  5. Mwanzo 10:5takriban 2247 KK

    (Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)

  6. Mwanzo 10:6takriban 2228 KK

    Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.

  7. Mwanzo 10:7takriban 2228 KK

    Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani.

  8. Mwanzo 10:8takriban 2289 KK

    Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani.

  9. Mwanzo 10:9takriban 2289 KK

    Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.”

  10. Mwanzo 10:10takriban 2259 KK

    Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari.

  11. Mwanzo 10:11takriban 2304 KK

    Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala,

  12. Mwanzo 10:12takriban 2304 KK

    na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.

  13. Mwanzo 10:13takriban 2304 KK

    Misraimu alikuwa baba wa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,

  14. Mwanzo 10:14takriban 2304 KK

    Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.

  15. Mwanzo 10:15takriban 2304 KK

    Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,

  16. Mwanzo 10:16takriban 2304 KK

    Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

  17. Mwanzo 10:17takriban 2304 KK

    Wahivi, Waariki, Wasini,

  18. Mwanzo 10:18takriban 2304 KK

    Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika,

  19. Mwanzo 10:19takriban 2304 KK

    na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

  20. Mwanzo 10:20takriban 2304 KK

    Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

  21. Mwanzo 10:21takriban 2304 KK

    Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

  22. Mwanzo 10:22takriban 2304 KK

    Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

  23. Mwanzo 10:23takriban 2304 KK

    Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

  24. Mwanzo 10:24takriban 2304 KK

    Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, naye Shela akamzaa Eberi.

  25. Mwanzo 10:25takriban 2247 KK

    Eberi akapata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.