Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Tongue

56 mistari · 6 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. (Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)

  2. Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

  3. Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja.

  4. Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari nao wakaishi huko.

  5. Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali.

  6. Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.”

  7. Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga.

  8. Bwana akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao.

  9. Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”

  10. Hivyo Bwana akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji.

  11. Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote.

  12. Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia.

  13. Wakati maneno ni mengi, dhambi haikosekani, lakini yeye ambaye huzuia ulimi wake ni mwenye busara.

  14. Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.

  15. Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake hujilinda na maafa.

  16. Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.

  17. wakati wa kurarua na wakati wa kushona, wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza,

  18. “Nami, kwa sababu ya matendo yao na mawazo yao, niko karibu kuja na kukusanya mataifa yote na lugha zote, nao watakuja na kuuona utukufu wangu.

  19. Siku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja.

  20. Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.

  21. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao.

  22. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.

  23. Basi walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu.

  24. Waliposikia sauti hii, umati wa watu ulikusanyika pamoja wakistaajabu, kwa sababu kila mmoja wao aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.

  25. Wakiwa wameshangaa na kustaajabu wakauliza, “Je, hawa wote wanaozungumza si Wagalilaya?