Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Tongue

56 mistari · 6 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

  2. Kwa ulimi tunamhimidi Bwana, yaani Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.

  3. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haistahili kuwa hivyo.

  4. Je, chemchemi yaweza kutoa katika tundu moja maji matamu na maji ya chumvi?

  5. Je, ndugu zangu, mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Wala chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.

  6. Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao.