- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1446–1406 BC
The Wilderness Years
Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.
Mistari ya kipindi hiki
- Hesabu 31:16takriban 1452 KK
“Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasi Bwana kwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu wa Bwana.
- Hesabu 31:17takriban 1452 KK
Sasa waue wavulana wote. Pia muue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa,
- Hesabu 31:18takriban 1452 KK
lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.
- Hesabu 31:19takriban 1452 KK
“Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.
- Hesabu 31:20takriban 1452 KK
Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”
- Hesabu 31:21takriban 1452 KK
Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari waliokuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayo Bwana alimpa Mose:
- Hesabu 31:22takriban 1452 KK
Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi,
- Hesabu 31:23takriban 1452 KK
na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.
- Hesabu 31:24takriban 1452 KK
Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”
- Hesabu 31:25takriban 1452 KK
Bwana akamwambia Mose,
- Hesabu 31:26takriban 1452 KK
“Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa.
- Hesabu 31:27takriban 1452 KK
Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya.
- Hesabu 31:28takriban 1452 KK
Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya Bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo au mbuzi.
- Hesabu 31:29takriban 1452 KK
Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya Bwana.
- Hesabu 31:30takriban 1452 KK
Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Bwana.”
- Hesabu 31:31takriban 1452 KK
Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose.
- Hesabu 31:32takriban 1452 KK
Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000,
- Hesabu 31:33takriban 1452 KK
ngʼombe 72,000,
- Hesabu 31:34takriban 1452 KK
punda 61,000,
- Hesabu 31:35takriban 1452 KK
na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.
- Hesabu 31:36takriban 1452 KK
Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa: Kondoo 337,500
- Hesabu 31:37takriban 1452 KK
ambayo ushuru kwa ajili ya Bwana ilikuwa kondoo 675;
- Hesabu 31:38takriban 1452 KK
ngʼombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa ngʼombe 72;
- Hesabu 31:39takriban 1452 KK
punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa punda 61;
- Hesabu 31:40takriban 1452 KK
Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa watu 32.