Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 31:41takriban 1452 KK

    Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

  2. Hesabu 31:42takriban 1452 KK

    Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani,

  3. Hesabu 31:43takriban 1452 KK

    nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500,

  4. Hesabu 31:44takriban 1452 KK

    ngʼombe 36,000,

  5. Hesabu 31:45takriban 1452 KK

    punda 30,500,

  6. Hesabu 31:46takriban 1452 KK

    na wanadamu 16,000.

  7. Hesabu 31:47takriban 1452 KK

    Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Bwana.

  8. Hesabu 31:48takriban 1452 KK

    Kisha maafisa waliokuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Mose

  9. Hesabu 31:49takriban 1452 KK

    na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana.

  10. Hesabu 31:50takriban 1452 KK

    Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa Bwana vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za Bwana.”

  11. Hesabu 31:51takriban 1452 KK

    Mose na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakshiwa.

  12. Hesabu 31:52takriban 1452 KK

    Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimletea Bwana kama zawadi ilikuwa shekeli 16,750

  13. Hesabu 31:53takriban 1452 KK

    Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi.

  14. Hesabu 31:54takriban 1452 KK

    Mose na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana.

  15. Hesabu 32:1takriban 1452 KK

    Kabila la Wareubeni na Wagadi, waliokuwa na makundi makubwa ya ngʼombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo.

  16. Hesabu 32:2takriban 1452 KK

    Hivyo walimjia Mose, na kuhani Eleazari na viongozi wa jumuiya, na kuwaambia,

  17. Hesabu 32:3takriban 1452 KK

    “Atarothi, Diboni, Yazeri, Nimra, Heshboni, Eleale, Sebamu, Nebo na Beoni,

  18. Hesabu 32:4takriban 1452 KK

    nchi ambayo Bwana ameishinda mbele ya wana wa Israeli, inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo.

  19. Hesabu 32:5takriban 1452 KK

    Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, nchi hii na ipewe watumishi wako kama milki yetu. Usitufanye tuvuke Yordani.”

  20. Hesabu 32:6takriban 1452 KK

    Mose akawaambia Wagadi na Wareubeni, “Je, watu wa nchi yenu watakwenda vitani wakati ninyi mmeketi hapa?

  21. Hesabu 32:7takriban 1452 KK

    Kwa nini mmewakatisha Waisraeli tamaa wasivuke katika nchi ambayo Bwana amewapa?

  22. Hesabu 32:8takriban 1452 KK

    Hivi ndivyo baba zenu walivyofanya wakati nilipowatuma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza nchi.

  23. Hesabu 32:9takriban 1452 KK

    Baada ya kufika kwenye Bonde la Eshkoli na kuitazama nchi, waliwakatisha tamaa Waisraeli wasiingie katika nchi ambayo Bwana alikuwa amewapa.

  24. Hesabu 32:10takriban 1452 KK

    Siku ile hasira ya Bwana iliwaka naye akaapa kiapo hiki:

  25. Hesabu 32:11takriban 1452 KK

    ‘Kwa kuwa hawakunifuata kwa moyo wote, hakuna mtu yeyote mwenye miaka ishirini au zaidi ambaye alikuja kutoka Misri atakayeona nchi niliyoahidi kwa kiapo kwa Abrahamu, Isaki na Yakobo;