Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 32:37takriban 1452 KK

    Nao Wareubeni wakajenga upya miji ya Heshboni, Eleale na Kiriathaimu,

  2. Hesabu 32:38takriban 1452 KK

    pia Nebo na Baal-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa) na Sibma. Miji waliyoijenga upya waliipa majina.

  3. Hesabu 32:39takriban 1452 KK

    Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori waliokuwa huko.

  4. Hesabu 32:40takriban 1452 KK

    Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko.

  5. Hesabu 32:41takriban 1452 KK

    Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi.

  6. Hesabu 32:42takriban 1452 KK

    Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.

  7. Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni.

  8. Kwa agizo la Bwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:

  9. Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote,

  10. waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.

  11. Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.

  12. Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.

  13. Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.

  14. Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.

  15. Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.

  16. Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.

  17. Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.

  18. Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.

  19. Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.

  20. Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.

  21. Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.

  22. Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.

  23. Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.

  24. Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.

  25. Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.