Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.

  2. Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.

  3. Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.

  4. Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.

  5. Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.

  6. Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Mose,

  7. “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani,

  8. wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada.

  9. Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki.

  10. Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.

  11. “ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.

  12. Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

  13. Hesabu 34:1takriban 1452 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  14. Hesabu 34:2takriban 1452 KK

    “Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:

  15. Hesabu 34:3takriban 1452 KK

    “ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi,

  16. Hesabu 34:4takriban 1452 KK

    katiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni,

  17. Hesabu 34:5takriban 1452 KK

    mahali ambapo utapinda, na kuunganika na Kijito cha Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati.

  18. Hesabu 34:6takriban 1452 KK

    “ ‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.

  19. Hesabu 34:7takriban 1452 KK

    “ ‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori,

  20. Hesabu 34:8takriban 1452 KK

    na kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi,

  21. Hesabu 34:9takriban 1452 KK

    kuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hasar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.

  22. Hesabu 34:10takriban 1452 KK

    “ ‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hasar-Enani hadi Shefamu.

  23. Hesabu 34:11takriban 1452 KK

    Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.

  24. Hesabu 34:12takriban 1452 KK

    Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi. “ ‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’ ”

  25. Hesabu 34:13takriban 1452 KK

    Mose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. Bwana ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu,