Rukia maudhui

circa 1446–1406 BC

The Wilderness Years

Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.

2,247 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hesabu 34:14takriban 1452 KK

    kwa sababu jamaa ya kabila la Reubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase wamekwishapokea urithi wao.

  2. Hesabu 34:15takriban 1452 KK

    Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ngʼambo ya Yeriko, kuelekea mawio ya jua.”

  3. Hesabu 34:16takriban 1452 KK

    Bwana akamwambia Mose,

  4. Hesabu 34:17takriban 1452 KK

    “Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni.

  5. Hesabu 34:18takriban 1452 KK

    Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi.

  6. Hesabu 34:19takriban 1452 KK

    Haya ndiyo majina yao: “Kalebu mwana wa Yefune, kutoka kabila la Yuda;

  7. Hesabu 34:20takriban 1452 KK

    Shemueli mwana wa Amihudi, kutoka kabila la Simeoni;

  8. Hesabu 34:21takriban 1452 KK

    Elidadi mwana wa Kisloni, kutoka kabila la Benyamini;

  9. Hesabu 34:22takriban 1452 KK

    Buki mwana wa Yogli, kiongozi kutoka kabila la Dani;

  10. Hesabu 34:23takriban 1452 KK

    Hanieli mwana wa Efodi, kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;

  11. Hesabu 34:24takriban 1452 KK

    Kemueli mwana wa Shiftani, kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;

  12. Hesabu 34:25takriban 1452 KK

    Elisafani mwana wa Parnaki, kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;

  13. Hesabu 34:26takriban 1452 KK

    Paltieli mwana wa Azani, kiongozi kutoka kabila la Isakari;

  14. Hesabu 34:27takriban 1452 KK

    Ahihudi mwana wa Shelomi, kiongozi kutoka kabila la Asheri;

  15. Hesabu 34:28takriban 1452 KK

    Pedaheli mwana wa Amihudi, kiongozi kutoka kabila la Naftali.”

  16. Hesabu 34:29takriban 1452 KK

    Hawa ndio watu ambao Bwana aliamuru wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

  17. Hesabu 35:1takriban 1451 KK

    Bwana akamwambia Mose katika nchi tambarare ya Moabu, kando ya Mto Yordani kuvukia Yeriko,

  18. Hesabu 35:2takriban 1451 KK

    “Waagize Waisraeli kuwapa Walawi miji ya kuishi kutoka urithi ambao Waisraeli wataumiliki. Wape maeneo ya malisho kuzunguka hiyo miji.

  19. Hesabu 35:3takriban 1451 KK

    Kisha watakuwa na miji ya kuishi na maeneo ya malisho kwa ajili ya ngʼombe zao, mbuzi, kondoo na mifugo yao mingine yote.

  20. Hesabu 35:4takriban 1451 KK

    “Maeneo ya malisho kuzunguka miji hiyo ambayo mtawapa Walawi yataenea mita 450 kutoka kwenye ukuta wa miji.

  21. Hesabu 35:5takriban 1451 KK

    Nje ya mji, pima mita 900 upande wa mashariki, upande wa kusini mita 900, upande wa magharibi mita 900, na upande wa kaskazini mita 900, na mji utakuwa katikati. Eneo hili litakuwa lao kwa ajili ya malisho.

  22. Hesabu 35:6takriban 1451 KK

    “Miji sita mtakayowapa Walawi itakuwa ya makimbilio, ambayo mtu anayemuua mwenzake aweza kukimbilia humo. Zaidi ya hiyo, wapeni miji mingine arobaini na miwili.

  23. Hesabu 35:7takriban 1451 KK

    Kwa jumla inawapasa kuwapa Walawi miji arobaini na minane, pamoja na maeneo ya malisho yao.

  24. Hesabu 35:8takriban 1451 KK

    Miji ambayo mtawapa Walawi kutoka nchi ambayo Waisraeli wanamiliki itatolewa kwa uwiano wa urithi wa kila kabila. Chukua miji mingi kutoka lile kabila lenye miji mingi, lakini uchukue miji michache kutoka kwa kabila lile lenye miji michache.”

  25. Hesabu 35:9takriban 1451 KK

    Kisha Bwana akamwambia Mose: