- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 605–538 BC
The Babylonian Exile
Jerusalem falls and the temple burns; Ezekiel and Daniel minister among the exiles as Lamentations mourns the city's ruin.
Mistari ya kipindi hiki
- Maombolezo 4:16takriban 588 KK
Bwana mwenyewe amewatawanya; hawaangalii tena. Makuhani hawaonyeshwi heshima, wazee hawakubaliki.
- Maombolezo 4:17takriban 588 KK
Zaidi ya hayo, macho yetu yalichoka, kwa kutazamia bure msaada; tuliangalia kutoka minara yetu kwa taifa lisiloweza kutuokoa.
- Maombolezo 4:18takriban 588 KK
Watu walituvizia katika kila hatua hata hatukuweza kutembea katika barabara zetu. Mwisho wetu ulikuwa karibu, siku zetu zilikuwa zimetimia, kwa maana mwisho wetu ulikuwa umefika.
- Maombolezo 4:19takriban 588 KK
Waliotufuatia walikuwa wepesi kuliko tai angani; walitusaka juu milimani na kutuvizia jangwani.
- Maombolezo 4:20takriban 588 KK
Mpakwa mafuta wa Bwana, pumzi ya uhai wetu hasa, alinaswa katika mitego yao. Tulifikiri kwamba chini ya kivuli chake tungeliweza kuishi miongoni mwa mataifa.
- Maombolezo 4:21takriban 588 KK
Shangilia na ufurahi, ee Binti Edomu, wewe unayeishi nchi ya Usi. Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa, Utalewa na kuvuliwa nguo ubaki uchi.
- Maombolezo 4:22takriban 588 KK
Ee Binti Sayuni, adhabu yako itaisha, hatarefusha muda wako wa kukaa uhamishoni. Lakini, ee Binti Edomu, ataadhibu dhambi yako, na atafunua uovu wako.
- Maombolezo 5:1takriban 588 KK
Kumbuka, Ee Bwana, yaliyotupata, tazama, nawe uione aibu yetu.
- Maombolezo 5:2takriban 588 KK
Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zetu kwa wageni.
- Maombolezo 5:3takriban 588 KK
Tumekuwa yatima wasio na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane.
- Maombolezo 5:4takriban 588 KK
Ni lazima tununue maji tunayokunywa, kuni zetu zapatikana tu kwa kununua.
- Maombolezo 5:5takriban 588 KK
Wanaotufuatilia wapo kwenye visigino vyetu, tumechoka na hakuna pumziko.
- Maombolezo 5:6takriban 588 KK
Tumejitolea kwa Misri na Ashuru tupate chakula cha kutosha.
- Maombolezo 5:7takriban 588 KK
Baba zetu walitenda dhambi na hawapo tena, na sisi tunachukua adhabu yao.
- Maombolezo 5:8takriban 588 KK
Watumwa wanatutawala na hakuna wa kutuokoa mikononi yao.
- Maombolezo 5:9takriban 588 KK
Tunapata chakula chetu kwa kuhatarisha maisha yetu kwa sababu ya upanga jangwani.
- Maombolezo 5:10takriban 588 KK
Ngozi yetu ina joto kama tanuru, kwa sababu ya fadhaa itokanayo na njaa.
- Maombolezo 5:11takriban 588 KK
Wanawake wametendwa jeuri katika Sayuni, na mabikira katika miji ya Yuda.
- Maombolezo 5:12takriban 588 KK
Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, wazee hawapewi heshima.
- Maombolezo 5:13takriban 588 KK
Vijana wanataabika kwenye mawe ya kusagia, wavulana wanayumbayumba chini ya mizigo ya kuni.
- Maombolezo 5:14takriban 588 KK
Wazee wameondoka langoni la mji, vijana wameacha kuimba nyimbo zao.
- Maombolezo 5:15takriban 588 KK
Furaha imeondoka mioyoni mwetu, kucheza kwetu kumegeuka maombolezo.
- Maombolezo 5:16takriban 588 KK
Taji imeanguka kutoka kichwani petu. Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!
- Maombolezo 5:17takriban 588 KK
Kwa sababu hiyo, mioyo yetu inazimia, kwa sababu ya hayo, macho yetu yamefifia,
- Maombolezo 5:18takriban 588 KK
kwa ajili ya Mlima Sayuni, ambao unakaa ukiwa, nao mbweha wanatembea juu yake.