Rukia maudhui

circa 605–538 BC

The Babylonian Exile

Jerusalem falls and the temple burns; Ezekiel and Daniel minister among the exiles as Lamentations mourns the city's ruin.

1,784 mistari · 3 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Maombolezo 3:57takriban 588 KK

    Ulikuja karibu nilipokuita, nawe ukasema, “Usiogope.”

  2. Maombolezo 3:58takriban 588 KK

    Ee Bwana, ulichukua shauri langu, ukaukomboa uhai wangu.

  3. Maombolezo 3:59takriban 588 KK

    Umeona, Ee Bwana, ubaya niliotendewa. Tetea shauri langu!

  4. Maombolezo 3:60takriban 588 KK

    Umeona kina cha kisasi chao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu.

  5. Maombolezo 3:61takriban 588 KK

    Ee Bwana, umesikia matukano yao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu:

  6. Maombolezo 3:62takriban 588 KK

    kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia dhidi yangu mchana kutwa.

  7. Maombolezo 3:63takriban 588 KK

    Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama, wananidhihaki katika nyimbo zao.

  8. Maombolezo 3:64takriban 588 KK

    Uwalipe kile wanachostahili, Ee Bwana, kwa yale ambayo mikono yao imetenda.

  9. Maombolezo 3:65takriban 588 KK

    Weka pazia juu ya mioyo yao, laana yako na iwe juu yao!

  10. Maombolezo 3:66takriban 588 KK

    Wafuatilie katika hasira na uwaangamize kutoka chini ya mbingu za Bwana.

  11. Maombolezo 4:1takriban 588 KK

    Jinsi dhahabu ilivyopoteza mngʼao wake, dhahabu iliyo safi haingʼai! Vito vya thamani vimetawanywa kwenye mwanzo wa kila barabara.

  12. Maombolezo 4:2takriban 588 KK

    Wana wa Sayuni wenye thamani, ambao mwanzo uzito wa thamani yao ulikuwa wa dhahabu, sasa wanaangaliwa kama vyungu vya udongo, kazi ya mikono ya mfinyanzi!

  13. Maombolezo 4:3takriban 588 KK

    Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto wao, lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma kama mbuni jangwani.

  14. Maombolezo 4:4takriban 588 KK

    Kwa sababu ya kiu ulimi wa mtoto mchanga umegandamana na kaakaa la kinywa chake, watoto huomba mkate, lakini hakuna yeyote awapaye.

  15. Maombolezo 4:5takriban 588 KK

    Wale waliokula vyakula vya kifahari ni maskini barabarani. Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau sasa wanalalia majivu.

  16. Maombolezo 4:6takriban 588 KK

    Adhabu ya watu wangu ni kubwa kuliko ile ya Sodoma, ambayo ilipinduliwa ghafula bila kuwepo mkono wa msaada.

  17. Maombolezo 4:7takriban 588 KK

    Wakuu wao walikuwa wamengʼaa kuliko theluji na weupe kuliko maziwa, miili yao ilikuwa myekundu kuliko marijani, kuonekana kwao kama yakuti samawi.

  18. Maombolezo 4:8takriban 588 KK

    Lakini sasa ni weusi kuliko masizi; hawatambulikani barabarani. Ngozi yao imeshikamana juu ya mifupa yao, imekuwa mikavu kama fimbo.

  19. Maombolezo 4:9takriban 588 KK

    Wale waliouawa kwa upanga ni bora kuliko wale wanaokufa njaa; wanateseka kwa njaa, wanatokomea kwa kukosa chakula kutoka shambani.

  20. Maombolezo 4:10takriban 588 KK

    Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye huruma wanapika watoto wao wenyewe, waliokuwa chakula chao watu wangu walipoangamizwa.

  21. Maombolezo 4:11takriban 588 KK

    Bwana ametoa nafasi kamilifu ya ghadhabu yake; ameimwaga hasira yake kali. Amewasha moto katika Sayuni ambao umeteketeza misingi yake.

  22. Maombolezo 4:12takriban 588 KK

    Wafalme wa dunia hawakuamini, wala mtu yeyote wa duniani, kwamba adui na watesi wangeweza kuingia kwenye malango ya Yerusalemu.

  23. Maombolezo 4:13takriban 588 KK

    Lakini hili lilitokea kwa sababu ya dhambi za manabii wake, na maovu ya makuhani wake, waliomwaga ndani yake damu ya wenye haki.

  24. Maombolezo 4:14takriban 588 KK

    Sasa wanapapasa papasa barabarani kama watu ambao ni vipofu. Wamenajisiwa kabisa kwa damu, hata hakuna anayethubutu kugusa mavazi yao.

  25. Maombolezo 4:15takriban 588 KK

    Watu wanawapigia kelele, “Ondokeni! Ninyi ni najisi! Ondokeni! Ondokeni! Msituguse!” Wanapokimbia na kutangatanga huku na huko, watu miongoni mwa mataifa wanasema, “Hawawezi kukaa hapa zaidi.”