Rukia maudhui

circa 605–538 BC

The Babylonian Exile

Jerusalem falls and the temple burns; Ezekiel and Daniel minister among the exiles as Lamentations mourns the city's ruin.

1,784 mistari · 3 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Maombolezo 3:7takriban 588 KK

    Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito.

  2. Maombolezo 3:8takriban 588 KK

    Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, anakataa kupokea maombi yangu.

  3. Maombolezo 3:9takriban 588 KK

    Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, amepotosha njia zangu.

  4. Maombolezo 3:10takriban 588 KK

    Kama dubu aviziaye, kama simba mafichoni,

  5. Maombolezo 3:11takriban 588 KK

    ameniburuta kutoka njia, akanirarua na kuniacha bila msaada.

  6. Maombolezo 3:12takriban 588 KK

    Amevuta upinde wake na kunifanya mimi niwe lengo kwa ajili ya mishale yake.

  7. Maombolezo 3:13takriban 588 KK

    Alinichoma moyo wangu kwa mishale iliyotoka kwenye podo lake.

  8. Maombolezo 3:14takriban 588 KK

    Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote, wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa.

  9. Maombolezo 3:15takriban 588 KK

    Amenijaza kwa majani machungu na kunishibisha kwa nyongo.

  10. Maombolezo 3:16takriban 588 KK

    Amevunja meno yangu kwa changarawe, amenikanyagia mavumbini.

  11. Maombolezo 3:17takriban 588 KK

    Amani yangu imeondolewa, nimesahau kufanikiwa ni nini.

  12. Maombolezo 3:18takriban 588 KK

    Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Bwana.”

  13. Maombolezo 3:19takriban 588 KK

    Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, uchungu na nyongo.

  14. Maombolezo 3:20takriban 588 KK

    Ninayakumbuka vyema, nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.

  15. Maombolezo 3:21takriban 588 KK

    Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini.

  16. Maombolezo 3:22takriban 588 KK

    Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.

  17. Maombolezo 3:23takriban 588 KK

    Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu.

  18. Maombolezo 3:24takriban 588 KK

    Nimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.”

  19. Maombolezo 3:25takriban 588 KK

    Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake, kwa yule ambaye humtafuta;

  20. Maombolezo 3:26takriban 588 KK

    ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa Bwana.

  21. Maombolezo 3:27takriban 588 KK

    Ni vyema mtu kuchukua nira bado angali kijana.

  22. Maombolezo 3:28takriban 588 KK

    Na akae peke yake awe kimya, kwa maana Bwana ameiweka juu yake.

  23. Maombolezo 3:29takriban 588 KK

    Na azike uso wake mavumbini bado panawezekana kuwa na matumaini.

  24. Maombolezo 3:30takriban 588 KK

    Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu.

  25. Maombolezo 3:31takriban 588 KK

    Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali na Bwana milele.