Rukia maudhui

circa 605–538 BC

The Babylonian Exile

Jerusalem falls and the temple burns; Ezekiel and Daniel minister among the exiles as Lamentations mourns the city's ruin.

1,784 mistari · 3 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Maombolezo 3:32takriban 588 KK

    Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma, kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.

  2. Maombolezo 3:33takriban 588 KK

    Kwa maana hapendi kuwaletea mateso au huzuni watoto wa wanadamu.

  3. Maombolezo 3:34takriban 588 KK

    Kuwaponda chini ya nyayo wafungwa wote katika nchi,

  4. Maombolezo 3:35takriban 588 KK

    Kumnyima mtu haki zake mbele za Aliye Juu Sana,

  5. Maombolezo 3:36takriban 588 KK

    kumnyima mtu haki: Je, Bwana asione mambo kama haya?

  6. Maombolezo 3:37takriban 588 KK

    Nani awezaye kusema nalo likatendeka kama Bwana hajaamuru?

  7. Maombolezo 3:38takriban 588 KK

    Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana ndiko yatokako maafa na mambo mema?

  8. Maombolezo 3:39takriban 588 KK

    Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake?

  9. Maombolezo 3:40takriban 588 KK

    Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Bwana Mungu.

  10. Maombolezo 3:41takriban 588 KK

    Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu kwa Mungu mbinguni, na tuseme:

  11. Maombolezo 3:42takriban 588 KK

    “Tumetenda dhambi na kuasi nawe hujasamehe.

  12. Maombolezo 3:43takriban 588 KK

    “Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia; umetuchinja bila huruma.

  13. Maombolezo 3:44takriban 588 KK

    Unajifunika mwenyewe kwa wingu, ili pasiwe na ombi litakaloweza kupenya.

  14. Maombolezo 3:45takriban 588 KK

    Umetufanya takataka na uchafu miongoni mwa mataifa.

  15. Maombolezo 3:46takriban 588 KK

    “Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao wazi dhidi yetu.

  16. Maombolezo 3:47takriban 588 KK

    Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula, uharibifu na maangamizi.”

  17. Maombolezo 3:48takriban 588 KK

    Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, kwa sababu watu wangu wameangamizwa.

  18. Maombolezo 3:49takriban 588 KK

    Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma, bila kupata nafuu,

  19. Maombolezo 3:50takriban 588 KK

    hadi Bwana atazame chini kutoka mbinguni na kuona.

  20. Maombolezo 3:51takriban 588 KK

    Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu.

  21. Maombolezo 3:52takriban 588 KK

    Wale waliokuwa adui zangu bila sababu wameniwinda kama ndege.

  22. Maombolezo 3:53takriban 588 KK

    Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo na kunitupia mawe;

  23. Maombolezo 3:54takriban 588 KK

    maji yalifunika juu ya kichwa changu, nami nikafikiri nilikuwa karibu kukatiliwa mbali.

  24. Maombolezo 3:55takriban 588 KK

    Nililiitia jina lako, Ee Bwana, kutoka vina vya shimo.

  25. Maombolezo 3:56takriban 588 KK

    Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako kilio changu nikuombapo msaada.”