Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 36:28takriban 1756 KK

    Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani.

  2. Mwanzo 36:29takriban 1756 KK

    Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,

  3. Mwanzo 36:30takriban 1756 KK

    Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.

  4. Mwanzo 36:31takriban 1756 KK

    Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:

  5. Mwanzo 36:32takriban 1756 KK

    Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.

  6. Mwanzo 36:33takriban 1869 KK

    Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.

  7. Mwanzo 36:34takriban 1827 KK

    Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.

  8. Mwanzo 36:35takriban 1785 KK

    Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.

  9. Mwanzo 36:36takriban 1743 KK

    Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.

  10. Mwanzo 36:37takriban 1701 KK

    Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.

  11. Mwanzo 36:38takriban 1659 KK

    Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.

  12. Mwanzo 36:39takriban 1617 KK

    Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.

  13. Mwanzo 36:40takriban 1617 KK

    Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao: Timna, Alva, Yethethi,

  14. Mwanzo 36:41takriban 1617 KK

    Oholibama, Ela, Pinoni,

  15. Mwanzo 36:42takriban 1617 KK

    Kenazi, Temani, Mibsari,

  16. Mwanzo 36:43takriban 1617 KK

    Magdieli na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki. Huyu ndiye alikuwa Esau, baba wa Waedomu.

  17. Mwanzo 37:1takriban 1728 KK

    Yakobo akaishi Kanaani katika nchi ambayo baba yake alikuwa ameishi.

  18. Mwanzo 37:2takriban 1728 KK

    Zifuatazo ni habari za Yakobo. Yosefu, kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akichunga makundi ya kondoo na mbuzi pamoja na ndugu zake wa mama wengine, yaani wana wa Bilha na wana wa Zilpa wake za baba yake, naye akawa akimletea baba yake taarifa mbaya kuhusu hao ndugu zake.

  19. Mwanzo 37:3takriban 1728 KK

    Basi, Israeli akampenda Yosefu kuliko yeyote miongoni mwa kaka zake, kwani ni mwanawe wa uzeeni, akamshonea joho lililorembwa vizuri sana.

  20. Mwanzo 37:4takriban 1728 KK

    Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yosefu kuliko yeyote mwingine miongoni mwao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema.

  21. Mwanzo 37:5takriban 1728 KK

    Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi.

  22. Mwanzo 37:6takriban 1728 KK

    Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota:

  23. Mwanzo 37:7takriban 1728 KK

    Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.”

  24. Mwanzo 37:8takriban 1728 KK

    Ndugu zake wakamwambia, “Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?” Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia.

  25. Mwanzo 37:9takriban 1728 KK

    Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, “Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.”