Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 37:35takriban 1728 KK

    Wanawe wote na binti zake wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu mpaka nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia.

  2. Mwanzo 37:36takriban 1728 KK

    Wakati ule ule, Wamidiani wakamuuza Yosefu huko Misri kwa Potifa, mmojawapo wa maafisa wa Farao, aliyekuwa mkuu wa ulinzi.

  3. Mwanzo 38:1takriban 1739 KK

    Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake, akaenda kuishi na Hira Mwadulami.

  4. Mwanzo 38:2takriban 1739 KK

    Huko Yuda akakutana na binti wa Kikanaani aitwaye Shua, akamwoa na akakutana naye kimwili,

  5. Mwanzo 38:3takriban 1738 KK

    akapata mimba, akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri.

  6. Mwanzo 38:4takriban 1737 KK

    Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita Onani.

  7. Mwanzo 38:5takriban 1736 KK

    Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita Shela. Huyu alimzalia mahali paitwapo Kezibu.

  8. Mwanzo 38:6takriban 1736 KK

    Yuda akampatia Eri, mzaliwa wake wa kwanza, mke aitwaye Tamari.

  9. Mwanzo 38:7takriban 1736 KK

    Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana akamuua.

  10. Mwanzo 38:8takriban 1722 KK

    Kisha Yuda akamwambia Onani, “Kutana kimwili na mke wa ndugu yako, na utimize wajibu wako kwake kama mke wa ndugu yako, ili umpatie ndugu yako uzao.”

  11. Mwanzo 38:9takriban 1722 KK

    Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga chini mbegu za kiume ili asimpatie ndugu yake uzao.

  12. Mwanzo 38:10takriban 1722 KK

    Alichofanya kilikuwa kiovu machoni pa Bwana, hivyo, pia Bwana akamuua Onani.

  13. Mwanzo 38:11takriban 1722 KK

    Kisha Yuda akamwambia Tamari mkwewe, “Ishi kama mjane nyumbani mwa baba yako mpaka mwanangu Shela atakapokua.” Kwa maana alifikiri, “Angeweza kufa pia kama ndugu zake.” Kwa hiyo Tamari alikwenda kuishi nyumbani kwa baba yake.

  14. Mwanzo 38:12takriban 1722 KK

    Baada ya muda mrefu mke wa Yuda binti wa Shua akafariki. Baada ya msiba, Yuda alikwenda Timna, kwa watu waliokuwa wakikata kondoo wake manyoya, naye alifuatana na rafiki yake Hira Mwadulami.

  15. Mwanzo 38:13takriban 1722 KK

    Tamari alipoambiwa, “Baba mkwe wako yuko njiani kwenda Timna kukata kondoo wake manyoya,”

  16. Mwanzo 38:14takriban 1722 KK

    alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.

  17. Mwanzo 38:15takriban 1722 KK

    Yuda alipomwona alifikiri ni kahaba, kwa sababu alikuwa amefunika uso wake.

  18. Mwanzo 38:16takriban 1722 KK

    Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.” Yule mkwewe akamuuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?”

  19. Mwanzo 38:17takriban 1722 KK

    Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.” Akamuuliza, “Utanipa kitu chochote kama amana mpaka utakapompeleka?”

  20. Mwanzo 38:18takriban 1722 KK

    Akamuuliza, “Nikupe amana gani?” Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake.

  21. Mwanzo 38:19takriban 1722 KK

    Tamari akaondoka, akavua shela yake akavaa tena nguo zake za ujane.

  22. Mwanzo 38:20takriban 1722 KK

    Wakati ule ule, Yuda akamtuma rafiki yake Mwadulami apeleke yule mwana-mbuzi ili arudishiwe amana yake kutoka kwa yule mwanamke, lakini yule rafiki yake hakumkuta yule mwanamke.

  23. Mwanzo 38:21takriban 1722 KK

    Akawauliza watu wanaoishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa kuabudia miungu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?” Wakamjibu, “Hajawahi kuwepo mwanamke yeyote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.”

  24. Mwanzo 38:22takriban 1722 KK

    Kwa hiyo akamrudia Yuda na kumwambia, “Sikumpata. Zaidi ya hayo, watu wanaoishi mahali pale walisema ‘Hapakuwahi kuwepo mwanamke yeyote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.’ ”

  25. Mwanzo 38:23takriban 1722 KK

    Kisha Yuda akasema, “Mwache avichukue vitu hivyo, ama sivyo tutakuwa kichekesho. Hata hivyo, nilimpelekea mwana-mbuzi, lakini hukumkuta.”