Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 37:10takriban 1728 KK

    Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako na mimi na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe hadi nchi?”

  2. Mwanzo 37:11takriban 1728 KK

    Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni.

  3. Mwanzo 37:12takriban 1728 KK

    Basi, ndugu zake walikuwa wamekwenda kuchunga makundi ya baba yao karibu na Shekemu,

  4. Mwanzo 37:13takriban 1728 KK

    naye Israeli akamwambia Yosefu, “Kama ujuavyo, ndugu zako wanachunga makundi huko karibu na Shekemu. Njoo, nitakutuma kwao.” Yosefu akajibu, “Vema sana, niko tayari.”

  5. Mwanzo 37:14takriban 1728 KK

    Kwa hiyo akamwambia, “Nenda uone kama mambo yote ni salama kwa ndugu zako na makundi, kisha uniletee habari.” Ndipo akamtuma Yosefu kutoka Bonde la Hebroni. Yosefu alipofika Shekemu,

  6. Mwanzo 37:15takriban 1728 KK

    mtu mmoja akamkuta akizungukazunguka mashambani na akamuuliza, “Unatafuta nini?”

  7. Mwanzo 37:16takriban 1728 KK

    Akajibu, “Ninawatafuta ndugu zangu. Unaweza kuniambia wanachunga wapi makundi yao?”

  8. Mwanzo 37:17takriban 1728 KK

    Yule mtu akajibu, “Wamehama hapa. Nilisikia wakisema, ‘Twende Dothani.’ ” Kwa hiyo Yosefu akawafuatilia ndugu zake na kuwakuta karibu na Dothani.

  9. Mwanzo 37:18takriban 1728 KK

    Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga shauri baya la kumuua.

  10. Mwanzo 37:19takriban 1728 KK

    Wakaambiana, “Yule mwota ndoto anakuja!

  11. Mwanzo 37:20takriban 1728 KK

    Njooni sasa, tumuue na kumtupa katika shimo mojawapo na tuseme kwamba mnyama mkali amemrarua. Kisha tutaona matokeo ya ndoto zake.”

  12. Mwanzo 37:21takriban 1728 KK

    Reubeni aliposikia jambo hili, akajaribu kumwokoa kutoka mikononi mwao akasema, “Tusiutoe uhai wake.

  13. Mwanzo 37:22takriban 1728 KK

    Tusimwage damu yoyote. Mtupeni katika shimo lililoko hapa jangwani, lakini msimguse.” Reubeni alisema hivyo ili amwokoe kutoka mikononi mwao, kisha amrudishe nyumbani kwa baba yake.

  14. Mwanzo 37:23takriban 1728 KK

    Kwa hiyo Yosefu alipowafikia ndugu zake, walimvua lile joho lake, lile joho lililorembwa vizuri alilokuwa amevaa.

  15. Mwanzo 37:24takriban 1728 KK

    Kisha wakamchukua wakamtupa katika shimo. Wakati huo shimo lilikuwa tupu, halikuwa na maji ndani yake.

  16. Mwanzo 37:25takriban 1728 KK

    Walipokaa ili wale chakula chao, wakainua macho wakaona msafara wa Waishmaeli ukija kutoka Gileadi. Ngamia wao walikuwa wamepakizwa mizigo ya vikolezo, uvumba na manemane, nao walikuwa njiani kuvipeleka Misri.

  17. Mwanzo 37:26takriban 1728 KK

    Yuda akawaambia ndugu zake, “Tutafaidi nini ikiwa tutamuua ndugu yetu na kuificha damu yake?

  18. Mwanzo 37:27takriban 1728 KK

    Njooni, tumuuze kwa hawa Waishmaeli. Tusimguse, kwa kuwa hata hivyo yeye ni ndugu yetu, nyama yetu na damu yetu wenyewe.” Ndugu zake wakakubali.

  19. Mwanzo 37:28takriban 1728 KK

    Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri.

  20. Mwanzo 37:29takriban 1728 KK

    Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake.

  21. Mwanzo 37:30takriban 1728 KK

    Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?”

  22. Mwanzo 37:31takriban 1728 KK

    Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu.

  23. Mwanzo 37:32takriban 1728 KK

    Wakalichukua lile joho lililorembwa vizuri na kulipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeliokota hili joho. Uchunguze uone kama ni la mwanao.”

  24. Mwanzo 37:33takriban 1728 KK

    Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande.”

  25. Mwanzo 37:34takriban 1728 KK

    Kisha Yakobo akararua nguo zake, akavaa nguo ya gunia na kumwombolezea mwanawe kwa siku nyingi.