Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 36:3takriban 1796 KK

    pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi.

  2. Mwanzo 36:4takriban 1796 KK

    Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli,

  3. Mwanzo 36:5takriban 1796 KK

    Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani.

  4. Mwanzo 36:6takriban 1740 KK

    Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake.

  5. Mwanzo 36:7takriban 1740 KK

    Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao.

  6. Mwanzo 36:8takriban 1740 KK

    Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri.

  7. Mwanzo 36:9takriban 1740 KK

    Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri.

  8. Mwanzo 36:10takriban 1774 KK

    Haya ndiyo majina ya wana wa Esau: Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.

  9. Mwanzo 36:11takriban 1734 KK

    Wana wa Elifazi ni: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.

  10. Mwanzo 36:12takriban 1734 KK

    Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau.

  11. Mwanzo 36:13takriban 1734 KK

    Wana wa Reueli ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.

  12. Mwanzo 36:14takriban 1712 KK

    Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni: Yeushi, Yalamu na Kora.

  13. Mwanzo 36:15takriban 1712 KK

    Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni: Temani, Omari, Sefo, Kenazi,

  14. Mwanzo 36:16takriban 1712 KK

    Kora, Gatamu na Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Ada.

  15. Mwanzo 36:17takriban 1712 KK

    Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.

  16. Mwanzo 36:18takriban 1712 KK

    Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni: Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana.

  17. Mwanzo 36:19takriban 1712 KK

    Hawa ndio waliokuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hawa ndio waliokuwa wakuu wao.

  18. Mwanzo 36:20takriban 1806 KK

    Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,

  19. Mwanzo 36:21takriban 1800 KK

    Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.

  20. Mwanzo 36:22takriban 1756 KK

    Wana wa Lotani walikuwa: Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.

  21. Mwanzo 36:23takriban 1756 KK

    Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.

  22. Mwanzo 36:24takriban 1756 KK

    Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.

  23. Mwanzo 36:25takriban 1756 KK

    Watoto wa Ana walikuwa: Dishoni na Oholibama binti wa Ana.

  24. Mwanzo 36:26takriban 1756 KK

    Wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

  25. Mwanzo 36:27takriban 1756 KK

    Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani.