Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Praise

490 mistari · 106 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Sauti za shangwe na ushindi zinavuma hemani mwa wenye haki: “Mkono wa kuume wa Bwana umetenda mambo makuu!

  2. Nifungulie malango ya haki, nami nitaingia na kumshukuru Bwana.

  3. Hili ni lango la Bwana ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.

  4. Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu.

  5. Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.

  6. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  7. Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki.

  8. Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.

  9. Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu, nifundishe sheria zako.

  10. Ninakusifu mara saba kwa siku, kwa ajili ya sheria zako za haki.

  11. Midomo yangu na ibubujike sifa, kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.

  12. Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, kwa kuwa amri zako zote ni za haki.

  13. Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, na sheria zako zinitegemeze.

  14. Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.

  15. Wimbo wa kwenda juu. Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.

  16. Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu Bwana.

  17. Msifuni Bwana. Lisifuni jina la Bwana, msifuni, enyi watumishi wa Bwana,

  18. ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.

  19. Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.

  20. Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana; ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana;

  21. ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana; ninyi mnaomcha, msifuni Bwana.

  22. Msifuni Bwana kutoka Sayuni, msifuni yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Bwana.

  23. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.

  24. Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele.

  25. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.