Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Praise: His mercy

32 mistari · 106 vipengele

Mistari kuhusu His mercy

Chuja kwa kitabu
  1. Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia Bwana na kumsifu katika utukufu wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema: “Mshukuruni Bwana kwa kuwa upendo wake wadumu milele.”

  2. Utenzi wa Ethani Mwezrahi. Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele; kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako ujulikane kwa vizazi vyote.

  3. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  4. Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  5. Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  6. Wote wamchao Bwana na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  7. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.

  8. Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele.

  9. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.

  10. Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele.

  11. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.

  12. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele.

  13. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele.

  14. Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele.

  15. Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele.

  16. Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele.

  17. Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele.

  18. Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele.

  19. Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.

  20. Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele.

  21. Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.

  22. Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele.

  23. Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.

  24. Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.

  25. Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele.