Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Praise: All creation

11 mistari · 106 vipengele

Mistari kuhusu All creation

  1. Msifuni Bwana. Msifuni Bwana kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni.

  2. Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.

  3. Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.

  4. Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga.

  5. Vilisifu jina la Bwana kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.

  6. Aliviweka mahali pake milele na milele, alitoa amri ambayo haibadiliki milele.

  7. Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,

  8. umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,

  9. ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote,

  10. wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao,

  11. Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!