Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Praise

490 mistari · 106 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

  2. Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

  3. Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee.

  4. Wimbo. Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

  5. Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko.

  6. Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

  7. Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana, katika umati mkubwa nitamsifu.

  8. Msifuni Bwana. Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.

  9. Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.

  10. Msifuni Bwana. Enyi watumishi wa Bwana msifuni, lisifuni jina la Bwana.

  11. Jina la Bwana na lisifiwe, sasa na hata milele.

  12. Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa.

  13. bali ni sisi tunaomtukuza Bwana, sasa na hata milele. Msifuni Bwana.

  14. Nimrudishie Bwana nini kwa wema wake wote alionitendea?

  15. Nitakiinua kikombe cha wokovu na kulitangaza jina la Bwana.

  16. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote.

  17. Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la Bwana.

  18. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote,

  19. katika nyua za nyumba ya Bwana, katikati yako, ee Yerusalemu. Msifuni Bwana.

  20. Msifuni Bwana, enyi mataifa yote; mtukuzeni yeye, enyi watu wote.

  21. Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, uaminifu wa Bwana unadumu milele. Msifuni Bwana.

  22. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.

  23. Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  24. Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”

  25. Wote wamchao Bwana na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.”