Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Praise

490 mistari · 106 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele.

  2. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.

  3. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele.

  4. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele.

  5. Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele.

  6. Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele.

  7. Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele.

  8. Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele.

  9. Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele.

  10. Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.

  11. Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele.

  12. Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele.

  13. Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele.

  14. Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.

  15. Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele.

  16. Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele.

  17. Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele.

  18. Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele.

  19. Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele.

  20. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, Fadhili zake zadumu milele.

  21. Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele.

  22. Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele.

  23. Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele.

  24. Zaburi ya Daudi. Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote, mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako.

  25. Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote.